Mashine zikichoronga mlima na malori yakibeba kifusi kwenye bonde
la mto Rufiji eneo la mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme la Julius
Nyerere (JNHPP-MW2115) Julai 17, 2020.
Na Mwandishi Wetu,
JNHPP
HATUA zote nane (8) za
utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa maji la Julius Nyerere
(JNHPP-MW2115) kwenye bonde la mto Rufiji unaendelea kwa kasi inayohitajika,
Mhandisi mkazi wa mradi huo Eng. Mushubila Kamuhabwa amewaambia waandishi wa
habari kwenye eneo la mradi Julai 17, 2020.
Eng. Kamuhabwa ametaja
hatua hizo kuwa ni ujenzi wa njia kubwa ya ardhini ya mchepuko wa maji (diversion tunnel), sehemu ya kufua
umeme (power house), ukuta
utakaotengeneza bwawa, eneo la kupokelea umeme unapozalishwa (Switch yard), power intake, barabara na
madaraja, saddle dams nne na kuchakata
mawe yanayotumika kutengeneza zege na mahitaji mengine.
“Mradi
huu wa JNHPP una miradi mingi ndani yake na yote iko katika hatua mbalimbali na
hatua hizo kama nilivyozitaja kwa pamoja ndiyo zinajenga mradi mmoja wa Julius
Nyerere Hydro Power Project Megawati 2115 katika hilo ujenzi unaendelea katika
maeneo yote hayo, mafundi wako kazini na wanaendelea na ujenzi kwa kasi kubwa
kama inavyohitajika.” Alisema Eng. Kamuhabwa.
Alisema jambo la
kufurahisha tayari mradi umeanza kuchangamsha uchumi wa nchi na kutolea mfano wakati
wakiweka zege kwenye njia ya kuchepusha maji (diversion tunnel, zaidi ya tani
200 za nondo zimetumika hii inafaidisha viwanda vyetu hapa nchini lakini pia wananchi
wanaokaa vijiji vinavyozunguka eneo la mradi wanafaidika kwa namna mbalimbali
ikiwwemo miundombinu wezeshi kama vile umeme unaotoka Morogoro kuja hapa
umepitia kwenye vijiji kadhaa natayari baadhi yao wameanza kufaidika na umeme
huo.” Alisema na kuongeza…Lingine zaidi ya vijana wa Kitanzania wapatao 4,000
kutoka maeneo mbalimbali nchini hususan yale yanayozunguka eneo la mradi
wameajiriwa na wanashiriki katika mradi kwa ari kubwa.
“Tunatarajia idadi hiyo
ya ajira ikaongezeka hadi kufikia watu 6,000 mradi utakapofikia hatua ya juu peak.” Alisema Eng. Kamuhabwa.
Kwa upande wao baadhi
ya wanakijiji wa Kisaki kilomita 60 kutoka eneo la mradi wamempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli kwa kuwaletea mradi huo
kwani tayari manufaa yake wameanza kuyaona.
“Kisaki
inakuja juu, tuna uhakika mradi ukimalizika Kisaki itakuwa kama Morogoro, kwa
sasa biashara inakuwa kwa kasi sana tofauti na hapo awali, mfano mchele tunauza
kwa kilo shilingi 1,600/= tofauti na hapo awali tulikuwa tunauza shilingi 500/=
bei ya juu kabisa shilingi 1,000/=, watu wameongezeka sana.” Alisema
mwanakijiji wa Kisaki Ali Matumbo na kuongeza…umeme nao tayari umefika kijijini
kwetu, shule imepata umeme kwa hivyo tunafuraha sana kwa ujio wa mradi huu na
tunampongeza sana Rais wetu Magufuli.
Naye mwanakijiji mwingine
Bi. Asha Said alisema, anauhakika hata barabara nzuri itajengwa kutokana na
mradi huo na anafurahi kuona wageni wengi wanafika Kisaki na hivyo biashara zao
zimechangamka.
Naye mwanakijiji
mwingine Hassan Mohammed Ngozi alisema, anayo matumaini makubwa kwa hali
anavyoiona hivi sasa hapo Kisaki, mradi utakapokamilika watakuwa na Kisaki
mpya.
“Kwetu
sisi ongezeko la watu hapa Kisaki limekuwa na faida kubwa………..watu wakienda kufanya
kazi huko kwenye mradi wanakuja hapa kijijini wananunua bidhaa zetu na sisi
tunapata pesa haya ni manufaa makubwa kwetu.” Alisema Bw. Ngozi.
No comments:
Post a Comment