HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2020

WAKULIMA WAWILI KIZIMBANI KWA KUDAIWA KUFANYABIASHARA ZA DAWA ZA KULEVYA

Wakulima wawili wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.


NA JANETH JOVIN


WAKULIMA wawili wakazi wa Mwandeti jijiji Arusha, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa zaidi ya kilo 1200.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali mbele ya Hakimu Mkazi Gwantwa Mwankuga imewataja washtakiwa hao kuwa ni Seuli Mollel na Losieku Mollel ambapo wote wanashtakiwa chini ya kifungu cha sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya sura ya 95 ya sheria za Tanzania.


Inadaiwa kuwa, Julai 8 mwaka 2020 kwa mashtaka ya uhujumu uchumi yaliyo sajiliwa Mahakamani hapo kama mashauri namba 50 na 51 ya mwaka 2020.

Inadaiwa kuwa, Juni 2020 katika kijiji cha Longilong wilayani Arumeru mkoani Arusha,  mshtakiwa  Seuli alikutwa na kilo 649.5 za dawa ya kulevya aina ya bangi huku mshitakiwa Losieku alikutwa na kilo 728.9 za dawa hizo za kulevya.

 Washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote  kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kusikilizwa Mahakama Kuu au kwa kupatiwa kibali kutoka kwa DPP.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 22, 2020 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa, watuhumiwa wamerudishwa rumande.

No comments:

Post a Comment

Pages