HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2020

WATANZANIA WATAKIWA KUPENDA BIDHAA ZINZOZALISHWA NCHINI

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jorenkyelitz Enterprises, Rachel Kingu, akizungumza na waandishi wa habari walipotembea banda la SIDO katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
 Moja ya bidhaa zinazozalishwa na Kampuni ya Jorenkyelitz Enterprises.



 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jorenkyelitz Enterprises, Rachel Kingu, akipanga bidhaa zake katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jorenkyelitz Enterprises, Rachel Kingu, akionesha bidhaa zinazozalishwa na kampuni yake.


  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jorenkyelitz Enterprises, Rachel Kingu, akipanga bidhaa zake katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jorenkyelitz Enterprises, Rachel Kingu, akizungumza na mteja aliyetembelea banda lao katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF). (Picha na Francis Dande)
 

Na Janeth Jovin


BIDHAA zinazotoka nje ya nchi zimedaiwa kupata masoko makubwa nchini na kukwamisha zinazozalishwa na wajasiriamali wadogo wazawa hivyo watanzania watakiwa kupenda bidhaa za kwao.

Mjasiriamali kutoka Kampuni ya Jorenkyelitz Enterprises, Rachel Kingu amesema wajasiriamali wadogo nchini wanakabiliwa na changamoti mbalimbali ikiwamo ya bidhaa zao kukosa masoko hapa nchini hali inayochangia watanzania wengi kupanda bidhaa zinazotoka nje ya nchi.

Kingu ambaye ndio Mkurugenzi wa kampuni hiyo, ameyasema hayo leo katika viwanja vya maonesho ya 44 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Amesema katika maonesho hayo wanauza sana bidhaa zao lakini changamoto ni pale yanapoisha kwani ukosa masoko katika maduka makubwa maarufu kama "Supermarket".

"Ukipeleka bidhaa Supermarket unakuta wanakataa kwa kutuambia kuwa wateja wao wanapenda siagi kutoka nje, ili tuondokane na tatizo hilo viongozi wetu wa Serikali na wadau mbalimbali wanapaswa kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kupanda bidhaa za kitanzania," amesema.

Amesema yeye amekuwa akiuza bidhaa zake katika maonesho mbalimbali ya biashara, kwenye mikusanyiko ya watu na katika baadhi ya maduka makubwa ya nafaka.

Kingu amesema bidhaa ambazo kampuni yake inatengeneza ni siagi ya korosho, mafuta yatokanayo na mbegu za maboga, unga wa mtama, uwele, ulezi, dona, ubuyu na unga wa ndizi mbichi.

Aidha amesema pamoja na kuuza bidhaa zake hizo amekuwa akikumbana na changamoto ya baadhi ya wateja wake kutomlipa kwa wakati pindi wanapochukua bidhaa.

"Pamoja na changamoto hizo lakini nimefanikiwa kutambulisha bidhaa zangu maeneo mengi ya nchi na ninatarajia kuwa na kampuni kubwa ambayo itazalisha bidhaa nyingi na kuzisambaza katika maeneo yote ya Tanzania na nje," amesema

No comments:

Post a Comment

Pages