HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 19, 2020

Watendaji Asasi za kiraia waliochukua fomu za vyama vya siasa kugombea, washauriwa kuachia nafasi zao

Mratibu wa kitaifa wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Onesmo Olengurumwa pamoja na Ofisa dawati la wanachama THRDC Joyce Eliezer wakikabidhi baadhi ya machipisho kutoka THRDC.
 
Na Janeth Jovin

Watendaji wa Asasi za Kiraia waliojihusisha na michakato ya awali ndani ya vyama vya siasa na hasa uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi mbalimbali wametakiwa kuachia nafasi zao kwani kuendelea kuzishikilia si jambo nzuri kwa sasa na halina afya kwa ustawi wa Azaki hapa nchini.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa amesema alimpongeza Rais JohnMagufuli kwa kusimamia utaratibu wa kiongozi kushika moja lakini pia alionesha hofu yake kwa watendaji wa Asasi za kiraia kujihusisha na michakato ya awali ndani ya vyama na hasa uchukuaji fomu kuwania kugombea nafasi mbali mbali.

Amesema mkurugenzi yeyote wa asasi za kiraia aliyechukua fomu za vyama vya siasa kuomba kuteuliwa na chama fulani kuwa mgombea na bado yupo ofisi anaendelea na majukumu yake anapaswa kuachia nafasi yake mara moja ili kuondoa migongano ya kimaslahi inayoweza kutokea.

“Kuna hatari ya tasnia hizi kuyumba au kuwa na watu ambao wanawaza tu nafasi za siasa na uteuzi’’ amesema Olengurumwa,akitaja tasnia ya Asasi za kiraia miongoni mwa zingine zinazoweza kuathiriwa na watendaji wake kujiingiza kwenye siasa kwa malengo ama maslahi mengine.

Kwa mujibu wa Olengururumwa, amesema sera ya THRDC ambayo pia baadhi ya wanachama wake wamechukuwa fomu inaelekeza waachie ngazi kabla ya kugombea nafasi za kisiasa na wanaendelea kufanyia kazi kitendo cha wanachama waliofanya hivyo bila kufuata sera hiyo.

“Uwezi ukawa Mkurugenzi au ofisa wa taasisi Fulani imekwenda kuchukua fomu alafu bado unaendelea kuwa katika nafasi yao hiyo katika hiyo taasisi, jambo hilo halilete utawala bora na inaweza kusababisha migongano ya kimaslahi,” amesema

Amesema ili kuondoa migongano ya kimaslahi na kuonesha kuwa kuna utofauti kati ya taasisi na anayekwenda kugombea basi anapaswa kuachia nafasi yake.

“Mtetezi yeyote wa haki za binadamu anayekwenda kugombea alafu anajua sera inavyosema basi huyo atakuwa amevunja misingi hiyo bora ya sera, niwaombe anayetaka kugombea atangaze na haashie nafasi yake akikosa afanye utaratibu mwingine wa kurudi,” amesema

 Wadau wengine wa Asasi za kiraia wanashauri kuwa ni vyema viongozi ama watumishi wangeachana kwanza na kazi zao ili wajiunge na siasa na si kwenda kwenye siasa kujaribu bahati kwa uhakika kuwa hata wakikosa bado wana kazi zingine,jambo ambalo linapingwa vikali.

No comments:

Post a Comment

Pages