Mabweni hayo ni Bweni la shule ya African Muslim iliyopo maeneo ya Kaloleni mkoani Kilimanjaro na bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Waadventista wa Sabato Tanzania iliyopo Usa river wilayani Arumeru Mkoani Arusha
Mkaguzi wa Jesi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jerimiah Mkomangi amethibitisha leo Oktoba 9,2020 kutokea kwa moto katika bweni hilo la shule ya African Muslim na kwamba ni mara ya tatu kwa shule hiyo kuungua kwa vipindi tofuati
Amesema kwenye tukio hilo hakuna majeruhi wala kifo kwa sababu wanafunzi waliondolewa mapema na kupelekwa sehemu salama ingawa vitu vyao ikiwemo magodoro, vitanda, nguo, madaftari na vitu vingine vimeteketea kwa moto.
Katika bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Waadventista wa Sabato limeteketea kwa moto jana mchana na kuunguza vifaa mbalimbali vya wanafunzi.
Imeelezwa kuwa moto huo umetokea wakati wanafunzi wa shule hiyo wakiwa madarasani na uchunguzi wa kupata chanzo cha moto huo bado unaendelea.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani Arumeru Mkaguzi Alhaji Kimaro ameeleza vifaa mbalimbali vya wanafunzi katika vyumba 14 vimeteketea kabisa na moto kati ya vyumba 30 vilivyopo katika bweni hilo.
Naye Mkuu wa shule hiyo Mborega Petro amewaomba wasamaria wema kuwasaidia kwa hali na mali wanafunzi ambao wamepoteza vifaa vyao vya matumizi ya kila siku ya shuleni hapo.
October 10, 2020
Home
Unlabelled
Mabweni mawili yateketea kwa moto
Mabweni mawili yateketea kwa moto
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment