HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 10, 2020

REDET kusambaza watazamaji wa Uchaguzi 3000 wa muda mfupi nchi nzima siku ya Uchaguzi

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kupitia idara yake ya Sayansi ya Siasa na utawala hasa kitengo cha Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET), imesema kuwa itasambaza waangalizi 3000 wa muda mfupi siku ya uchaguzi.

Imesema waangalizi hao watakuwa na kazi ya kufuatilia, kuangalia mwenendo mzima wa kupiga kura, kuhesabu na hatimaye kutangazwa mshindi.

Aidha REDET imesema kuwa tayari imeshawasambaza waangalizi wa muda mrefu wa uchaguzi 200 na wanaendelea na kazi katika mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 8, 2020 Mwenyekiti na Mkuu wa Watazamaji wa Uchaguzi kutoka REDET, Profesa Rwekaza Mukandala amesema UDSM kupitia kitengo hicho wameendeleza historia yao ya kuangalia kila uchaguzi ambao umekuwa ukifanyika hapa nchini.

“Kwa uchaguzi wa mwaka huu REDET tutakuwa na waangalizi wa uchaguzi nchi nzima na waangalizi wa muda mrefu wapo 200 ambao tayari wameshaanza kazi na katika siku ya uchaguzi yenyewe kutakuwa na waangalizi 3000.

“Waangalizi wetu hawa wa muda mfupi watasambazwa nchi nzima na watakuwa na kazi ya kufatilia na kuangalia mwenendo mzima wa kupiga kura, kuhesabu na hatimaye kutangazwa kwa mshindi,” amesema Prof. Mukandala

Hata hivyo amesema mpaka kufikia uchaguzi wa mwaka 2015 yapo maboresho kadhaa yamefanyika katika eneo la mwenendo mzima wa kuendesha uchaguzi hapa nchini.

“Maboresho hayo, ni uwepo wa mfumo wa kutayarisha daftari la kudumu la wapiga kura, huko nyuma tulikuwa hatuna daftari la kuduma hivyo kila uchaguzi ukifanyika lilikuwa likitayarishwa daftari na mfumo wake wala haukuwa mzuri kwani ilikuwa na mwanya wa kuruhusu watu wasiostahili kupiga kura kupigamfano wahamiaji.

“Kwa kweli haya mambo yalikuwa yakileta mikaanganyiko mingi lakini kuanzia mwaka 2005 wakati wa uchaguzi mpaka sasa hivi kumekuwa na maboresho makubwa ikiwamo kuwa na daftari la kudumu la wapiga kula ambalo ni la kidigitali,” amesema

Amesema daftari la kudumu la wapiga kura limepunguza kwa kiasi kikubwa udanganyifu hasa katika kujua nani apige kura na yupi asipige kura.

Hata hivyo amesema jeshi la polisi linapaswa kulinda usalama na mali za wannachi Katika kipindi chote cha kampeni.

No comments:

Post a Comment

Pages