Na Mwandishi Wetu
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimeanza utekelezaji wa mradi wa 'Wanawake Wanaweza'unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wanawake (UN-Women).
Akizindua mradi huo leo Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Rose Reuben alisema mradi huo una lengo kuu la utetezi wa haki za wanawake na watoto, kuongeza ushiriki was wanawake katika uongozi , kuondoa mifumo kandamizi inayochochea ukatili kwa makundi hayo maalum kwa kutumia vyombo vya habari.
"Katika kufanikisha lengo kuu la mradi huo, TAMWA itawajengea uwezo wanahabari katika kuripoti habari za jinsia na ufuatiliaji wa ushiriki wa wanawake katika uongozi na siasa, " alisema Rose.
Pia TAMWA itaendesha midahalo katika miko 16 ambayo ni Dar Es Salaam , Pwani, Morogoro, Dodoma , Singida , Tabora na Shinyanga.
Mengine no Mwanza , Mara , Mbeya, Ruvuma , Lindi na Mtwara .
Pia wilaya 112 za mikoa hiyo na kata 48 ndio maeneo yatakayotumika kama sampuli ya utekelezaji wa mradi.
No comments:
Post a Comment