Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akimpa mwanachi kitabu cha muongozo cha huduma kwa wateja aliyetembelea Wiki ya Huduma kwa Wateja Makao Makuu ya Mamlaka hiyo Barabara ya Samnujoma jijini Dar es Salaam.
Afisa masoko wa TCRA dorice Mhimbila akimuhumia mwananchi katika wiki ya Maadhimisho ya Wiki ya Wateja alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo.
Wananchi wakipata maelezo katika Makumbusho ya TCRA walipotembelea mamlaka hiyo katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Na Mwandishi Wetu
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto kutembelea makumbusho ya mawasiliano yanayoelezea maendeleo na ukuaji wa teknolojia za mawasiliano duniani na hakuna gharama ya kuingia katika Makumbusho hayo ni bure.
TCRA inaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kutoa wito kwa wazazi na shule pamoja na wananchi kwenda katika makumbusho ya Mamlaka kujifunza vitu mbalimbali vilivyotumika katika Mawasiliano kabla ya ukuaji wa Teknolojia ya Mawasiliano haijaanza.
Katika Maadhimisho hayo Mamlaka imejenga dawati maalum la kuhudumia wateja kutokana na huduma wanazozitoa.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mabel Masasi amesema Maadhimisho hayo wanatarajia kupata maoni yao katika utoaji wa huduma kwa Mamlaka na kuangalia kujipanga katika mikakati.
Amesema Maadhimisho hayo ya huduma kwa wateja hufanyika kwa mwaka mara moja hivyo ni fursa ya wadau kujitokeza na kutoa maoni
"Tunaendelea kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja tukilenga kupata maoni yao na kutembelea katika dawati maalum lililoanzishwa kwa ajili hiyo"amesema Mabel.
Hata hivyo katika kuadhimisha Maadhimisho hayo kuna mikakati mbalimbali imewekwa kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma Bora za Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment