HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 25, 2020

Hatimaye wabunge 19 wa Chadema waapishwa

 

Hatimaye Wabunge19 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamesalimu amri na kuamua kuwaapishwa rasmi na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai.

Baada ya kuwaapisha Spika Ndugai ameahidi kuwalinda, kuwatetea na kuwapa ushirikiano,ili kukamulisha jukumu la kikatiba  katika kuwatumikia wananchi.

Spika Ndugai amesema kuwa Novemba 20 mwaka huu alipokea barua kutoka tume ya taifa ya uchaguzi ikimjulisha uteuzi wa wabunge hao 19 wa viti maalum.

Wabunge hao walioapishwa ni pamoja na Halima Mdee, Grace Tendega, Ester Matiko, Cecilia pareso, Ester Bulaya, Agnester Kaizer, Nusra Hanje, Jesca kishoa, Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo

Wengine ni Asia Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majela,Stella Fihaya, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchester Lwamlaza.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wabunge wengine, Mbunge wa Viti maalum Halima Mdee  amesema kuwa watanzania  wanapaswa kuelewa kuwa nafasi hiyo haikutolewa kama hisani bali ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao chama chao kimeupata.

Mdee amewahakikishia wanachama wa CHADEMA kuwa wabunge hao watafanya kazi kwa uaminifu kipindi chote watakachokuwa Bungeni kwa kuweka mbele maslahi ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuilinda katiba ya chama chao.

Mbunge wa viti maalumu Ester Matiku amesema kuwa nadhani wote tunajua taratibu za viti maalumu za kuweza kufika kwa Mbunge wa kuteuliwa,kuna utaratibu ambao unaendelea ndani ya chama kupitia na baadae chama kinabariki na majina yanaenda kwenye tume ya taifa ya uchaguzi.

“Binafsi nilitaarifiwa na mamlaka husika kuwa  nimeteuliwa ndio maana nimefika hapa kuja kuapa”amesema Matiku.

Matiku amesema kuwa watatumia  nguvu zote,akili zote na kwa hekima zote kuhakikisha kuwa wanawakilisha chama vizuri ndani na nje ya bunge lakini pia kuwatetea watanzania amabao wengi wao wanaimani na chama hicho

Hata hivyo wabunge hao waviti maalum wameapishwa baada ya kupita siku 15 tangu kuanza kwa bunge la 12 Mkutano wa kwanza wa mwaka 2020 uzinduliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli

No comments:

Post a Comment

Pages