HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 25, 2020

Wahitimu waaswa kujihadhari na maambukizi ya virusi vya Ukimwi

KAIMU Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro Michael Weluse, amewaasa wahitimu wa fani 11 za ujuzi  katika  wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi  na Huduma (Kihonda RVTSC), kutunza nguvu kazi zao kwa kujihadhari na maambukizi ya virusi vya  Ukimwi.

Akizungumza  juzi mkoani Morogoro  katika sherehe ya Mahafali ya 31 ya Chuo cha Ufundi  Stadi (VETA) Mkoa wa Marogoro, Weluse amesema takwimu  zinaonyesha kwamba mkoa huo una  maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi  asilimia 4.2 hivyo kuna umuhimu  wa Uongozi wa Chuo  cha Veta kuwaelekeza vijana juu ya ugonjwa hilo.

Amesema vijana wanapaswa kuelekezwa juu ya mapambano ya ugonjwa huo wa Ukimwi ili kuweza kusaidia kupoteza nguvu kazi katika Taifa.

Amesema katika mpango wa maendeleo ya mwananchi wa kitanzania, serikali inaendelea kusisitiza watu wafanye  kazi kwani   maisha bora yanapatikana kwa kufanya kazi kwa ufanisi,ambapo ufanisi huo  unatakiwa   uimarishe maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

"Taifa linatambua umuhimu wa kuwepo kwa Vyuo vya Ufundi Stadi vyenye kuwaandaa wataalamu katika nyanja mbali mbali za ufundi kwani vyuo hivyo ni sehemu muhimu ya kuwaandaa vijana kukabiliana na soko la ajira na kusaidia vijana  kujiajiri wao wenyewe,"amesema Weluse

Aidha amewataka  madereva wa malori na mabasi kuwa wasikivu na wazingatie mafunzo wanayopewa ili waweze kuepusha ajali za barabarani pindi wamalizapo mafunzo yao

"Mafundi magari, Zana za kilimo, umeme wa magari, wakereza vyuma na vipuri mbali mbali, hakikisheni kuwa mnapotengeneza magari au vipuri vya magari basi ubora wa kazi mzifanyazo uzingatiwe,"alisema na kuongeza

"Mafundi wa fani za ujenzi, umeme wa majumbani pamoja na majokofu na viyoyozi, kumbukeni kuwa kazi zenu huwa zinaonekana kwa kila mtu hivyo kama nyumba itajengwa kwa kiwango kizuri, ninyi tayari mnakuwa ni  sehemu mojawapo ya kujitangaza na kujipatia ajira binafsi kwa urahisi zaidi,"amesema Weluse

Amesema kwa ufundi wa ushonaji nguo, mafundi hao anatakiwa kuwa na elimu  ya kuwa wabunifu zaidi ili kukabiliana na wauza nguo kuukuu (mitumba) na za kushonwa na mafundi wengine, wanatakiwa kuwe wabunifu zaidi katika kutengeneza aina mbali mbali za mavazi.

Kwa Upande wake,Mkuu wa Chuo hicho cha Kihonda RVTSC, Kashindye Maganga alisema jumla ya wahitimu 241 wakiwwmo wasichana 54 na wavulana 187 wamehitimu fani hizo katika  mahafali hayo.

Aidha amesema  kwa fani ya udereva kuna wanafunzi 43 wa kozi ya madereva wa awali, madereva ya magari ya abiria 16 ambao wanaendela na mafunzo pia kuna madereva wa magari makubwa 14 ambao wanahitimu.

"Matarajio ya Menejimenti ya Chuo,  Wafanyakazi, na hasa Walimu, kwamba kutokana na mafunzo waliyoyapata wahitimu hao, watakuwa wabunifu, waangalifu,waaminifu, hodari na kuwa   tayari kujiendeleza kwa mafunzo ya ngazi nyingine," amesema

Naye Msoma risala wa wahitimu hao, Zakaria Muya amesema  miongoni mwa changamoto ambayo wanakabiliana kwa sasa ni  ukosefu wa mashine za teknolojia mpya katika karakana zao na  katika kozi za udereva wa magari makubwa wanahitaji magari ya kisasa ili kufundishia kufuatana na teknolojia iliyopo.

No comments:

Post a Comment

Pages