Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Liwale, James Milanzi, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Wanakijij wa Kijiji Mtawatawa wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho kuona namna USMJ inavyotekelezwa kijijini hapo.Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Mtawatawa Benadetha Kitang'ita akitoa ufafanuzi wa namna USMJ ilifanya miujiza kijijini hapo.
Ofisa Misitu Wilaya ya Liwale mkoani LindiNassoro Mzui (wa tatu kulia), Ofisa Sera na Uraghabishi wa MJUMITA Elida Fundi (wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wasimamizi wa misitu wa Mbila baada ya kutembelea msitu huo ambao umekuwa na faida lukuki kwa wananchi.
NA SULEIMAN MSUYA, LIWALE
USIMAMIZI
Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ) unaoratibiwa na mashirika
mbalimbali na serikali umefanya miujiza katika vijiji vingi vya Wilaya
ya Liwale mkoani Lindi kikiwemo kijiji cha Mtawatawa.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Mtawatawa, Benadetha
Kitang'ita wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea
kijiji hicho ambacho kinashiriki kwenye miradi ya USMJ inayotekelezwa
wilayani Kilwa.
Waandishi
hao walifanya ziara ya siku tano katika mkoani ya Iringa na Lindi
kuangalia hali ya USMJ kupitia Mradi wa Kuhifadhi Misitu kwa Kuwezesha
Biashara Endelevu ya Misitu (CoFoREST) na uratibubu wa Mtandao wa Jamii
wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) na Shirika la Kuhifadhi Misitu
Asili Tanzania (TFCG) ambayo yanafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la
Uswisi (SDC).
Kitang'ita
ambaye ni Ofisa Kilimo wa kijiji hicho amesema kwa kipindi cha miaka
mitano kupitia USMJ wamefanikiwa kukusanya zaid ya shilingi milioni 379
ambapo asilimia 55 ya mapato hayo yametumika kwenye kijiji ambazo ni
zaidi ya shilingi milioni 200.
Amesema
fedha hizo zinatokana na uvunaji na uuzaji wa mazao ya misitu kwa mfumo
endelevu wa rasilimali misitu zilizopo Msitu wa Mbila.
Alisema kwa miaka mitano kijiji kimeweza kuchangia kwenye Halmashauri ya Liwale ambapo zaidi ya shilingi milioni 150 zimetolewa.
Akifafanua
maajabu ambayo yametokea Mtawatawa ni pamoja na kuchimba kisima chenye
urefu wa mita 75 kwa shilingi milioni 12 hivyo kuondoa adha ya maji.
"Pia
USMJ umewezesha ujenzi wa nyumba ya kuishi mtendaji kwa shilingi
milioni 28, choo cha ofisi ya kijiji kwa shilingi milioni 6,
tumekarabati jengo la Zahanati ya kijiji kwa shilingi milioni 24 ambalo
lilisimama kwa miaka saba.
Pia
tumenunua trekta kwa shilingi milioni 71 hivyo tunalitumia kwa kuongeza
tija ya uzalishaji pamoja na kufanya kazi ya kubeba mbao ambazo
zinavunwa kwa njia haramu," amesema.
Kitang'ita amesema trekta hiyo inatumika kukodishwa kwa ajili ya kulimia wananchi ambapo uzalishaji umeongezeka mara dufu.
"Trekta
imewezesha uzalishaji kuongezeka kwa kulima hekari 235 kwenye bonde la
kijiji na ukijumlisha na wananchi mmoja mmoja zaidi hekari 500 na
uzalishaji umeongezeka.
Kaimu mtendaji amesema maajabu mengine ya USMJ Mtawatawa ni ujenzi wa darasa moja ambalo limegharimu shilingi milioni 18.
"Kijiji
kimetumia fedha zitokanazo na USMJ kuajiri mwalimu ambaye analipwa
shilingi 200,000 kwa mwezi kwa miaka mitano lengo ni kukabiliana na
uhaba wa walimu kwani tuna walimu wanne tu," amesema.
Aidha amesema kijiji kimenunua pikipiki tatu kwa kutumia fedha za USMJ jambo ambalo linaongeza uhifadhi na ulinzi wa misitu.
Amesema
wametoa mchango kwenye Kituo cha Afya Kibutuka shilingi milioni 3 na
kuchangia shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Shule
ya Sekondari Kiangara.
"USMJ
imesaidia kuongeza ufaulu na ufanisi kwa wanafunzi ambapo tumechangia
fedha za kuweka wanafunzi katika kambi ambapo tumekuwa tukitoa shilingi
500,000 hivyo kuwapunguzia maumivu wazazi," amesema.
Kitang'ita amesema pia kijiji kimeweza kulipia kodi ya nyumba kwa ajili ya wauguzi wawili ambao hawana nyumba za kuishi.
Amebainisha kuwa maajabu ya USMJ Mtawatawa ni kijiji kuweza kulipa posho wajumbe wa kijiji na wahifadhi wa kamati ya maliasili.
"Sisi
tukikutana kwenye mkutano mkuu wa kijiji tunahakikisha tunapika chakula
na kuwapatia maji wajumbe wote hali ambayo inachangia ushiriki wa
wananchi wengi," amesema.
Ofisa
Kilimo huyo amesema katika vijiji 72 vya wilaya ya Liwale Mtawatawa
imefanikiwa kupitia USMJ hivyo kuahidi kuendeleza kwani faida wanaiona.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Mtawatawa Omary Shamte, amesema sekta ya misitu imeweza
kuwakomboa na pongezi kubwa ziende kwa Shirika la Limasi na Mradi wa
Kuongeza Mnyororo wa Thamani kwenye Mazao ya Misitu (FORVAC).
"FORVAC
na Limasi wametufungua macho hivyo ujio wa CoFoREST kupitia MJUMITA na
TFCG ni jambo jema kwani watagusa matamanio yetu," amesema.
Kindamba Machwiiko Mzee wa Kijiji cha Mtawatawa, amesema uhifadhi unapaswa kuungwa mkono kwa kuwa una faida kubwa kwa wananchi.
Ofisa
Misitu Wilaya ya Liwale, Nassoro Mzui amesema wilaya hiyo ina vijiji 27
ambavyo vinajihusisha na USMJ katika msitu wa Angai.
Amesema idara yake imekuwa ikifanya vizuri kupitia USMJ kwani jamii imekuwa ikinufaika hivyo kushiriki kuilinda.
Mzui amesema ipo changamoto kubwa ambayo inachangiwa na ukumbwa wa misitu hivyo ulinzi kudororo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Wilaya ya Liwale, James Milanzi amesema ujio wa CoFoREST
na miradi mingine ni muhimu kwani unachochea kukuza uchumi, maendeleo na
uhifadhi.
Milanzi
amesema miradi hiyo inapunguzia jukumu halmashauri bajeti ya utekelezaji
miradi kama maji, afya, elimu na nyingine hivyo mpango wao ni kusambaza
wazo hilo la wadau kwa kutumia fedha za halmashauri.
Ofisa
Sera na Uraghibishi wa MJUMITA, Elida Fundi amesema ziara hiyo ya siku
tano iliyonzia Kijiji cha Mahenge, wilayani Kilolo mkoani Iringa hadi
Darajani na Mtawatawa wilayani Liwale ina lengo la kujifunza na kutoa
taarifa za USMJ ilivyo na faida kwa jamii.
Fundi amesema dhana hiyo ya USMJ imepokelewa kwa mtazamo chanya kwani maendeleo na uhifadhi umeonekana kuwa mzuri.
"Ziara hii imeonesha tunachokipigania kina matokeo chanya kwa wanavijiji kusema wenyewe faida ni nyingi kuliko hasara," amesema.
Fundi
ameitaka Serikali kuhamasisha na kutoa elimu ili dhana ya USMJ
inasambaa nchini kote ili kukusuru vijiji ambavyo vina misitu ila haina
mipango ya kuihifadhi kwa njia endelevu.
No comments:
Post a Comment