HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 26, 2020

WAKULIMA WA MPUNGA BONDE LA MTO RUFU KUNUFAINIKA NA PEMBEJEO KUTOKA BENKI YA TADB

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kati kati akiwa ameshika mkasi kwa ajili ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mradi wa mikopo ya pembejeo za kilimo ikiwemo matreka mawili katika halfa iliyofanyika katika ofisi za Chauru zilizopo Ruvu, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa na kulia kwake ni Mkurugenzi wa fedha wa benki wa wakulima ya TADB Delick Lugemala.

 

 VICTOR MASANGU, PWANI

 

 WAKULIMA zaidi ya elfu 3000 wanaolima   zao la mpunga  katika bonde la mto ruvu Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani   waliokuwa  wanakabiliwa na changamoto  kwa kipindi kirefu  hatimaye wamepata mkombozi baada ya serikali Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB)  kuja na  mpango wa  kuwaondolea  wimbi la umasikini kwa kuwawezesha kiuchimi.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evariost Ndikilo wakati wa halfa ya Makabidhiano ya  mkopo  matrekta mawili pamoja na  pembejeo nyingine za za kilimo  zenye thamani ya  kiasi cha shilingi milioni 480 kwa kwa uongozi wa chama cha ushirika  wa wakulima wa umwagiliaji wa ruvu (CHAURU)  ambayo imetolewa na benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB).

“Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani lengo letu kubwa kama serikali lazima tujitahidi kw ahali na mali kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo katika kuhakikisha kwamba wakulima wetu wanawezeshwa kiuchumi na kupatiwa mikopo ya bei nafuu lengo ikiwa ni kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini,”alisema Ndikilo.

Pia Mkuu huyo alisisitiza kuwa katika kufanikisha azma ya mradi huo mkubwa wa bonde la mto ruvu ataendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha wakulima wote wa mazao mbali mbali ikiwemo mpunga na kuwahimiza wadau wengine wa sekta ya kilimo kuweza kuunga juhudi za serikali katika kuwasaidia wakulima waweze kutimiza malengo waliyojiwekea,

Naye Mkurugenzi wa fedha wa benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Delick Lugemala ambaye ambaye  alimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuwakomboa wakulima kwa kuwapatia mikopo kwa bei nafuu na kwamba katika Mkoa mzima wa Pwani hadi sasa wameshatoa kiais cha shilingi zaidi ya bilioni 20.

Kadhalika Mkurugenzi huyo alisema kwamba lengo lao kubwa ni kuendelea kushirikiana na wakulima wa mazo mbali mbali katika kuwasapoti mitaji mbali mbali ya fedha ambayo watakuwa wanaipata kwa liba nafuu lengo ni kuwapatia fursa mbali mbali z akilimo amabzo zitawasaidia katika kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi hivyo benki itaendelea kuwasaidia kwa hali na mali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya chama cha ushirika wa wakulima wa umwagilianji Ruvu (CHAURU) Sadala Chacha amebainisha pembejeo hizo walizozipata na benki ya TADB ikiwemo matreka mawili  yataweza  kuwaondolea changamoto  kubwa za   upatikanaji wa zana za kilimo na kuwaondolea hali ya usumbufu waliokuwa wanaupata.

“Kwa kweli Mkuu wa Mkoa tunapenda sana kushukuru msaada huu ambao tumepatiwa kwani hapo awali tulikuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa pembejeo za kilimo hivyo kupelekea baadhi ya wananchama wetu kushindwa kutekeleza majukumu yao ipsasavyo kwa hiyo hii fursa tuliyoipata kwetu ni mkombozi mkubwa kutoka benki ya TADB,”alisema Mwenyekitu huyo.

Pia katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kutokana na mkopo huo walioupata kutoka benki ya TADB wanachama wake wataweza kupata fursa mbali mbali za kuwezeshwa kupata pembejeo za kilimi kwa wakati na bila ya kuwategemea baadhi ya walanguzi ambao wamekuwa wakiuziwa mchele huo kwa bei ambayo sio rafiki.

No comments:

Post a Comment

Pages