HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2020

Siku ya Kimataifa ya Maadhimisho ya Watetezi Wanawake wa Haki za Binadamu Yafanyika Dar es Salaam

 Na Talib Ussi, Zanzibar


Mrajisi wa Asasi za Kiraia (NGO), Tanzazia bara ameahidi kurekebisha mapungufu yaliyokuwemo kwenye sera na sheria ili kuwaondolea wanawake vikwazo vinavyopelekea kuwakandamiza katika harakati za maisha yao.


Akizungumza kwa niamba ya Mraji wa NGO Bw. Mussa Sang’anya katika  siku ya kimataifa ya maadhimisho ya watetezi wanawake wa haki za binadamu ambayo yamefanyika jana katika Ukumbi wa New Afrika Dar es  Salaam amesema Mrajisi amauagiza aseme/aeleze kwamba ofisi ya Mrajisi ipo tayari kushurika na asasi za kiraia kurekebisha mapungu yaliyokuwemo kwenye sera.


Pia amesema kupitia maadhimisho hayo ameelimika mambo mengi ambayo wanawake wanakumbana nayo ikiwemo kupigwa, kutelekezwa na kunyimwa haki zao hivyo serikali ya Tanzania ipo tayari kushirina na asasi zakirai hata katika kuboresha sheria mabli mbali za nchi.


“ Kikao hichi kimenielimisha mambo mengi ambayo wanawake wanakumbana nayo na kukwamisha harakati zao za maisha, pia nimealewa juhudi kubwa ambazo wanawake wa watetezi wanazozichukuwa kuwatetea wanawake wenzao, napenda kuweka wazi mrajis ameniagiza nisema ofisi yake iko wazi kushirikiana na NGOs kurekebisa sera hata katika kuboresha sheria, na serikali ipo tayari” Alisema Sang’nya.


Mapena wanaharakati walisimulia changamoto ambazo wanawake wanakumbana nazo ikiwemo rushwa ya ngozo, kudharauliwa kwakuwa ni mwanamke, kutomiliki mali, kupigwa, kunyimwa kupazwa sauti zao nk.


Akizungumza msilimuliaji Dkt, Helen Kijo Bisimba alisema kazi ya utetezi inahitaji kujitolewa na kuwa na sauti moja na kuangalia mazingira yaliyopo sasa. Amesema chagamoto kubwa inawakabili wanawake watetezi wanapofanya kazi yao utetezi ikwemo wanawake wenyewe kutojua kama watatetewa hivyo, ametoa wito kwa watetezi kutovujika moyo na kuelewa kwamba  kazi utetezi ni ya kujitolea nahitaji uvumilivu.


Naye mwenyekiti wa mtandao wa wanawake watete wa haki za Bidamu Bi Flaviana Charles ametowa wito kwa wanawake ambao wametendewa viendo vya ukatili ikiwemo kukatwa mikono, kupigwa na kunyanyaswa kusimama imara wakati watetezi wanawatetea kwa kuwa nao bega kwa bega.
Aida Mwenyekiti huyo amefurahiswa na kauli ya Mraji wa NGO ya kushirikian nao kurekebisha sera na sheria jambo ambalo litaweza kusaidia katika kutatua matatizo na vikwazo vingi vinayowakabili wanawake.

No comments:

Post a Comment

Pages