HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 21, 2021

SHIGONGO ATOA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA WATOTO WENYE MAHITAJI


OFISI ya Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, kupitia kamati yake ya kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shule, imeanza zoezi la kugawa sare za shule na madaftari kwa wanafunzi  wanaotoka kwenye familia duni zisizo na uwezo pamoja na watoto yatima.
 
Zoezi hilo limeanza leo Alhamisi, Januari 21, 2020 katika Shule ya Msingi Katwe, jimboni humo kwa kamati hiyo kushirikiana na Diwani wa Kata ya Katwe, Maximillian Mkungu, pamoja na uongozi wa shule na serikali za vijiji ikiwa ni wiki chache tangu kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari kote nchini.
 
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Didas Lunyungu amesema zoezi la ugawaji wa sare za shule pamoja na madaftari litakuwa endelevu na awamu hii inahusisha wanafunzi wanaotoka familia zisizo na uwezo ambao wanagawiwa sare za shule na madaftari huku wanafunzi wote wa darasa la kwanza katika Jimbo wakipewa madaftari.
 
Aidha, ameongeza kuwa lengo kubwa la kampeni hiyo iliyopewa jina la Kampeni ya Buchosa Mpya, Peleka Mtoto Shule na kauli mbiu yake ya ELIMU BORA KWA KILA MTOTO,  ni kutoa hamasa kwa wazazi kuwapeleka watoto wao shule ili wakapate elimu na watoto hao kusoma kwa bidii kwa manufaa yao ya baadaye na taifa kwa jumla pamoja na kuhamasisha kuinua kiwango cha elimu katika jimbo hilo.
 
Dk. Lunyungu amesema  Shigongo amedhamiria kuleta maendeleo ya kweli katika Jimbo la Buchosa ikiwa ni pamoja na kuinua kiwango cha elimu katika shule za msingi na sekondari jimboni humo.

No comments:

Post a Comment

Pages