HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 16, 2021

UTATA BABA MZAZI WA DIAMOND


Naseeb Abdul 'DiamondPlatnumz' 

 

 

 

Na Mwandishi Wetu

 

MSANII wa muziki kutoka nchini Tanzania Naseeb Abdul maarufu kama DiamondPlatnumz ameendelea kushika headlines katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii baada ya mama yake kusema ukweli kuhusu baba yake mzazi.

 

Kupitia kipindi cha Mashamsham kinachorushwa na redio ya Wasafi, Mohamed Salum maarufu kama ‘ricardomomo’ alijitambulisha rasmi kuwa yeye na Diamond ni mtu na kaka yake na kusema kuwa baba yao ni mmoja lakini mama ni tofauti.

 

“Nilitambulishwa kuwa Naseeb ni mdogo wangu na baba yetu mzazi ambaye ni marehemu kwa sasa, Mzee Salum Iddi Nyange hivyo mimi na Naseeb ni mtu na kaka kabisa” Alisema Ricardomomo.

 

Pia aliendelea kusema “watu wengi wamekuwa wakitaka sana kujua undugu wangu na Diamond umetoka wapi lakini nilikuwa nikisubiri wakati sahihi ufike ndio niseme ukweli, Naseeb ni mtoto wa Salum Iddi Nyange na sio mzee Abdul kama wengi wanavyojuwa, yule ni baba yake mlezi tu”.

 

Akithibitisha taharifa hizo kwa njia ya simu mama mzazi wa Diamond, Sandrah (Mama dangote), alisema taarifa hizo ni za kweli kwani aliolewa na mzee Abdul akiwa na ujauzito wa Diamond na baada ya kujifungua Abdul alikataa kumlea mtoto na kumpelekea yeye kumlea peke yake.

 

“Niliolewa na Abdul nikiwa na ujauzito wa Naseeb, na alikuwa analijua hilo na hata mtoto alivozaliwa alikataa kumlea kwa sababu sio wa kwake, baba yake na Naseeb anaitwa Salum Iddi Nyange alikuwa akiishi Kariakoo ambaye ni  marehemu kwa sasa”. Alisema mama Dangote.

 

Baada ya kumtafuta mzee Abdul ambaye anafahamika kama baba mzazi wa Diamond na kumuuliza juu ya taarifa hiyo alisema amesikitishwa sana na uamuzi wa mama Diamond kutoa kauli kama hiyo kwenye vyombo vya habari bila kumshirikisha na kusema amemdhalilisha.

 

“Mimi nimeumia sana lakini kama ndio ameamua kusema hivyo basi, ninachokijua  mimi Nasseb ni mtoto wangu na ndio maana anatumia jina langu, kama alikuwa na baba yake kwa nini aliamua kutumia jina langu?, Najua mama yake amesema haya kwasababu ya mali lakini atambue kwamba sisi sote ni marehemu watarajiwa na mali zote tutaziacha duniani”. Alisema mzee Abdul

 

Pia aliendelea kusema kuwa “Kuanzia leo sitaki Naseeb atumie tena jina langu, kama ana baba mwingine basi atumie  jina lake na akiendelea kulitumia nitamfungulia mashtaka”.

No comments:

Post a Comment

Pages