HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 16, 2021

MTOTO WA SHILOLE APATA DARAJA LA KWANZA KIDATO CHA NNE

Na Mwandishi Wetu


Mwanamuziki na mjasiriamali kutoka nchini Tanzania Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole, ameonyesha furaha baada ya binti yake wa kwanza Joyce kufaulu vizuri katika mtihani wake wa kuhitimu kidato cha nne.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole ameandika “ Mwenyenzi Mungu asante, leo ni kati ya siku nilizowahi kuwa katika kiwango cha juu kabisa cha furaha na shukrani kwa Allah: MUNGU AMENITENDEA WEMA.

 

Mimi kama binti mwingine yeyote, nilikuwa na ndoto za kufanya vizuri shuleni lakini sikuwahi kufanikiwa katika hilo, njia yangu ilikuwa na miiba na mapito mengi, sifahamu hata cheti cha darasa la 7 kinaonekana vipi. Nilipokosa hayo nikaapa, nikamuomba Mungu na kuwekeza nguvu zangu kuhakikisha watoto wangu wanapita kwenye ile njia ambayo mimi sikuweza.

 

Joyce kama mtoto wangu wa kwanza ambaye kuzaliwa na kukuwa kwake kulikuwa kwa tabu zaidi, ninamuombea usiku na mchana aje kupita katika hizi njia za kisomi na kuwa mwanamke niliyewahi kuota. Mungu anaanza kujibu:

 

MWANANGU AMEFAULU VIZURI SANA, NIMEAMBIWA KAPATA ‘DIVISION ONE (1) YA POINT 16.

 

Nimelia, nimecheka, nimesimama, nimekaa ninamshukuru Mungu, nimshukuru binti yangu kwa kuendelea kunitoa aibu. I am proud of her. Nakupongeza sana mwanangu, nakupenda na kukuombea mafanikio zaidi, safari yako ndio kwanza inaanza. Allah azidi kukujalia.

 

Nawashukuru sana waalimu na wafanyakazi wa St.Christina kule Tanga, nawashukuru na kuwapongeza wanafunzi wote walioshirikiana na mwanangu kwenye masomo na Maisha ya shule”. Ameandika Shilole.

 

Aidha Shilole amewashukuru wateja wake wa shishifood na mashabiki wake wa muziki wanaomuwezesha na kupata fedha za kuwasomesha watoto wake.

No comments:

Post a Comment

Pages