HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 09, 2021

SERIKALI KILIMANJARO "YAIPIGIA CHAPUO" BENKI YA USHIRIKA (KCBL) KWA WAWEKEZAJI

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuiaga Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCBL iliyomaliza muda wake baada ya kuhudumu kwa muda wa miaka miwli .
Meneja Mkuu wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) Godfrey Ngura akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuiaga Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCBL ,Aziza Mshanga akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ya muda ya kupitia changamoto zilizkuwa zikiikabili Benki ya Ushirika Kilimanjaro Clement Kwayu akitoa taarifa wakati wa hafla fupi ya kuiaga bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo waliomaliza muda wao .
Meneja Mkuu wa Benki ya KCBL,Godfrey Ng'ura akikabidhi tuzo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira wakitambua mchango uliofanywa na kiongozi huyo katika kuipigania benki hiyo.
Meneja Mkuu wa Benki ya KCBL,Godfrey Ng'ura akikabidhi cheti kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira wakitambua mchango uliofanywa na kiongozi huyo katika kuipigania benki hiyo.
Meneja Mkuu wa Benki ya Ushirika (KCBL) Godfrey Ng'ura (kushoto) akikabidhi tuzo kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCBL iliyomaliza muda wake Aziza Mshanga wakati wa hafla fupi ya kuiaga bodi hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya KCBL waliomaliza muda wao .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) muda mfupi bada ya kuwaaga wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo waliomaliza muda wao.

 

Na Dixon Busagaga -Kilimanjaro

 

SERIKALI mkoani Kilimanjaro imepiga chapuo kwa wawekezaji nchini kununua hisa za Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) ili kuongeza mtaji hadi kufikia sh Bil 100 utakao saidia benki hiyo kuwa benki ya kitaifa kwa kusogeza huduma zake katika nchi nzima.

Hatua hiyo inatokana na Benki ya KCBL kuanza upya utoaji wa huduma baada ya changamoto mbalimbali ilizopitia na kupelekea kunusurika kuwa miongoni mwa Benki zilizofutwa na Benki kuu baada ya wadau na viongozi wa serikali kuweka juhudi za kuinusuru.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuiga Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira alisema

“Sisi ni mashahidi watu wameanza kuingia na kutoka ndani ya Benki na Benki inafanya vizuri ,tumeletewa wataalamu wazuri sana katika masuala ya benki ,na wanasimamaia utaratibu vizuri fedha zinazoingia na fedha zinazotoka lakini yutahitaji kukuza mitaji “alisema Dkt Mghwira

“Lengo letu sisi lilikuwa ni kufikia Bil 100 angalau ,uwe mtaji wa kuanzia kwa hiyo tulikuwa tunatafuta wawekezaji wakubwa ambao wangeweza kununua asilimia ishirini ,ishirini za Bil 20 za hisa kama watatu wanne ,ambao tulikuwa tunategemea kwa njia hiyo tungeweza kupata wawekezaji wakubwa  “aliongeza Dkt Mghwira .

Alisema serikali bado inaendelea kuwatafuta na kwamba upo uwezekana wakapataikana baada ya baadhi ya benki kubwa kuonesha nia ya kununua hisa katika benki hiyo hatua itakayosaidia kuongeza mtaji wa benki .

Meneja Mkuu wa Benki hiyo Godfrey Ng’ura alisema changamoto zilizokuwepo awali  katika benki hiyo kwa sasa zimemalizkka na kwamba tayari huduma imeanza kutolewa ambapo katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo  tayari akaunti mpya zaidi ya 200 zimefunguliwa .

“Benki inamtaji na ukwasi wa kutosha ,tumeemndelea kuwalipa wateja wetu amana zao , na watejawameendelea kufungua akaunti ,katika miezi mitatu tumefungua akaunti mpya zaidi ya 200 zenye thamani ya zaidi ya Mil 600 na tumefanya malipo katika amana za wateja ndani ya miezi mitatu zaidi ya Bilioni 2”alisema Ng’ura .

Benki ya Ushirika Kilimanjaro ilizinduliwa kwa mara nyingine hivi karibuni baada ya kuingia mkataba wa makubaliano na Benki ya CRDB  ambapo imefanya uwekezaji wa shilingi Bilioni 7kwa lengo la kuimarisha utendaji wa benki ya ushirika.

No comments:

Post a Comment

Pages