HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 12, 2021

Somo la Historia ya Tanzania kuanza kufundishwa Shuleni Mwezi Julai


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na waandisgi wa habari jijini Dodoma leo Februari 12, 2021.  


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na waandisgi wa habari jijini Dodoma leo Februari 12, 2021.  Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Dkt. Leonard Akwilapo. 

 

 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


SERIKALI imesema Somo la Historia ya Tanzania litaanza kutumika kwa lazima kuanzia mwezi Julai Mwaka huu lengo likiwa ni kuwajenga uwezo wanafunzi kuwa na uzalendo na kuwatambua mashujaa wote wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Wizara ya Elimu Dodoma.


Profesa Ndalichako amesema katika kuzingatia maelekezo ya Rais  wa Tanzania Dkt.John Magufuli, Somo hilo la Historia lisomwe na wanafunzi wote na mihtasari imeandaliwa kusoma somo hilo la Historia kuanzia Elimu ya awali na kuendelea kwa ulazima.

Aidha amesema Wizara inaendela kushirikiana na wadau mbalimbali kuchapisha vitabu na vitakamilika mwezi March mwaka huu ambapo Somo litaanza kufundishwa Mwezi Julai ,2021.

Katika hatua nyingine Profesa Ndalichako amebainisha kwamba Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia inashirikiana na wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo katika uandaji wa mihtasari.

"Nasisitiza watunzi wa vitabu Lazima wahakikishe wanaandika kwa ufasaha hivyo Sisi kama Wizara tunashirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo katika kuandika," amesema Profesa Ndalichako.

kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt Leonard Akwilapo amesema Somo la Historia ya Tanzania litafundishwa kwa lugha ya kiswahili kuanzia darasa la Saba hadi kidato cha Sita.

Ikumbukwe kuwa Rais wa Tanzania  Dkt John Magufuli
Wakati akiapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma mnamo tarehe 9 Desemba 2020 aliagiza Somo la Historia ya Tanzania lianze kufundishwa mashuleni ili kujenga uzalendo  na kuwafanya wanafunzi kujua walikotoka.

No comments:

Post a Comment

Pages