NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
SHIRIKISHO
la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA), limeiomba Serikali kuwaongeza
mshahara katika bajeti ya Mwaka huu Wafanyakazi katika sekta zote nchini
zikiwemo Sekta binafsi kwa lengo la kuwaboreshea maslahi watumishi.
Kauli
hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Rais wa Shirikisho hilo,Tumaini
Nyamuhoka wakati akifunga Kikao kazi kwa Makatibu wa Chama Cha
Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) yaliliyolenga kuwajengea uwezo.
"Tunampongeza
Rais Magufuli kwakuwarudisha kazini watumishi ambao wana Elimu ya
darasa la Saba huku akiomba kuwalipa mishara yao kwa kipindi ambacho
walikuwa hawapo kazini," amesema Nyamuhoka.
Katika
hatua nyingine ametoa wito kwa Wakurugenzi Halmashauri,Wakuu wa
Taasisi pamoja na Makatibu Tawala Nchini kuacha kuwadharau Viongozi wa
Wafanyakazi na badala yake wawape kipaumbele kwa kuwasikiliza .
Hata
hivyo amekemea suala la baadhi ya Maofisa kuwekwa ndani kutokana na
kuwapa Fedha Viongozi wao licha ya wao kutokuwa na makosa kutokana na
kuagizwa tu kufanya hivyo.
Kwa
upande wake Mweka Hazina wa Talgwu Taifa Siston Mizengo ameeleza
mafanikio yaliyopatikana kutokana na kuweza kutekeleza mipango yake
iliyojiwekea na kwasasa kipo vizuri na ilipata hati Safi.
No comments:
Post a Comment