HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 07, 2021

UWANGUTA KUFIKISHA KILIO KWA WAZIRI WA NISHATI KWA KUTOLIPWA FEDHA NGUZO KWA WAKATI

Mwenyekiti wa UWANGUTA Negro Sanga akiongea kwenye kikao cha kujadili safari ya kwenda kumuona waziri wa nishati kuelezea changamoto ya malipo kutoka katika kapuni ambazo hununua nguzo ambazo hazijawekwa dawa.
Baadhi ya wafabishara wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa wakiwa kwenye kikao cha kujadili safari ya kwenda kumuona waziri wa nishati kuelezea changamoto ya malipo kutoka katika kapuni ambazo hununua nguzo ambazo hazijawekwa dawa.

Baadhi ya wafabishara wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa wakiwa kwenye kikao cha kujadili safari ya kwenda kumuona waziri wa nishati kuelezea changamoto ya malipo kutoka katika kapuni ambazo hununua nguzo ambazo hazijawekwa dawa.


Na Fredy Mgunda, Iringa

 

 CHAMA cha wafanyabiashara wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa (UWANGUTA) wamepanga kupeleka kilio kwa waziri wa nishati kwa kutolipwa kwa wakati kutoka kwenye viwanda na makapuni ambayo yamekuwa yakinunua nguzo hizo kutoka kwa wafanyabiasha hao.

Akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabishara hao,mwenyekiti wa UWANGUTA Negro Sanga alisema kuwa makampuni ambayo yamekuwa yakinunua nguzo hizo yamekuwa yakiwacheleweshea malipo wafanyabisha hao na kuwa pelekea kupata hasara mara kwa mara.

 

Alisema wafanyabishara hao wanakutana na changamoto ya mitaji kutokana na kutegemea kukopa kwenye benki mbalimbali ili kuendesha biashara ya nguzo hivyo kucheleshwa kwa malipo kutoka kwenye kampuni hizo kunawasababishia kulimbikiza au kukua kwa riba katika benki ambazo wanakuwa wamekopa fedha hizo.

 

Sanga aliongeza kwa kusema kuwa lengo la kwenda kumuona waziri wa nishati Dr Medard Matogolo Kalemani ni kufikisha kilio cha kutolipwa kwa wakati kutoka kwenye kampuni ambazo wamekuwa wakiziuzia nguzo hizo tofauti na alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli alipokuwa kwenye ziara mkoani Iringa.

“Mheshimiwa Rais alitoa wiki mbili kuhakikisha kuwa sisi wafanyabisha wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa tuliambiwa tulipwe baada ya wiki mbilia ila hadi sasa bvaadhi yetu wamelipwa na wengine hadi hizi sasa tunavyoongea Zaidi ya wafabiashara mia moja (100) hawajalipwa fedha zao” alisema Sanga

 

Sanga alimalizia kwa kusema kuwa wameamua kwenda kwa waziri baada ya kufanya kila jitihada kushindikana kutatua changamoto hiyo ya kulipwa kwa wakati kama iliyokuwa miaka ya nyuma hivyo kwa pamoja wameamua kufunga safari kwa kwenda kutoa malalamiko kwa waziri wa nishati.

Nao baadhi ya wafanyabisha wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa waliomba serikali kuzitambua kampuni zote na viwanda ambavyo vinanua nguzo hizo kutoka kwa wafanyabisha hao ili kuondoa ubabaishaji kutoka kwenye kampuni hizo.

 

Walisema kuwa kampuni nyingi mara kwa mara husema kuwa hawajalipwa kutoka katika shirika la umeme Tanzania (TANESCO) hivyo kunasababisha kuwacheleweshea malipo hayo kwa wafanyabishara wa nguzo ambazo hazina dawa.

 

Waliongeza kuwa kuna baadhi ya wafanyabishara hao wa nguzo ambazo hazijawekwa dawa hawajalipwa toka mwaka jana 2020 mwezi wa tisa kutoa kwenye kampuni ya New forest iliyopo mkoani Iringa.

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Pages