HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 12, 2021

MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA SOKOINE KUFANYIKA SUA MOROGORO


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)  Prof. Maulid Mwatawala (wa kwanza kulia) akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo yatakayofanyika Chuoni hapo mwezi huu mwishoni kulia kwake ni Prof. Samweli Kaboto Mwenyekiti wa kamati ya mandalizi ya maadhimisho hayo.

Mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho hayo Prof. Samweli Kabote ( Wa kwanza kushoto)   akizungumzia maandalizi hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na waandishi wa habari. Katikati ni Prof. Maulid Mwatawala Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo na Mariam Mwayela.Wa kwanza kulia ni Afisa Mahusiano na Masoko wa SUA.


Afisa Mahusiano na Masoko wa SUA, Mariam Mwayela ( kulia) akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano huo wa waandishi wa habari,
Washiriki wa mkutano huo na Wandishi wa habari wakifuatilia taarifa inayotolewa kuhusu maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao
Mkutano ukiendelea.
Washiriki wa mkutano huo na Wandishi wa habari wakifuatilia taarifa inayotolewa kuhusu maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao.
Washiriki wa mkutano huo na Wandishi wa habari wakifuatilia taarifa inayotolewa kuhusu Maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao.
Mkutano ukiendelea.
 
 

Na Calvin Gwabara, Morogoro


CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeahidi kunedelea kuenzi mchango wa AliyekuwaWaziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine kutokana na ushupavu wake kama kiongozi katika kusimamia uchapakazi, Kilimo vijijini, Uzalendo na kuchukia rushwa.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala wakati akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo juu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Hayati Edward Moringe Sokoine kwa mwaka 2021.

“Chuo kiliamua kutekeleza maamuzi ya kuadhimisha siku hii kuanzia mwaka 1992 kwa kuwa kiongozi huyu alikuwa mchapa kazi na alipigania ,masuala ya kilimo hasa katika mapinduzi vijijini na utoshelevu wa chakula kwa watanzania” Alisisitiza Prof. Mwatawala.

Prof.Mwatawala aliongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wake Hayati Sokoine alipiga vita suala la rushwa na kuimarisha uadilifu katika utumishi wa umma ambapo serikali iliyopomadarakani inayazingatia na kuyaenzi kwa ajili ya maendeleo yaTaifa.

Kaimu Makamu huyo wa Mkuu wa Chuo alibainisha kuwa maadhimisho hayo kwa  mwaka huu yatafanyika kuanzia tarehe 24-27 Mei, 2021 chuoni hapo baada ya kuhairishwa hapo awali kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John PombeMagufuli.

Aidha alisema mambo yatakayofanyika katika wiki hiyo ya maonesho yateknolojia na ubunifu katika Kilimo, Ufugaji naUvuvi, kufanya mkutano  wakisayansi kwa wanataaluma, watafiti, wanafunzi na wadau mbalimbalii, mdahalo wa kitaifa wa kumbukizi  yaSokoineutakaofanyika siku ya tarehe 27 Mei 2021, kutoa huduma za afya kwa binadamu hususani magonjwa yasiyo ambukiza, kutoa huduma za tiba ya  mifugo 

kupitia  hospitali ya rufaa ya wanyama bure kwa jamii, kuchangia damu salama na kufanya michezo mbalimbali ambayo itaambatana na zawadi kwawashindi..

Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki dunia kwa ajali ya gari Aprili 12, 1984 akiwa na umri wa miaka 46 katikaMkoa wa Morogoro akitokea Dodoma katika kikao cha Bunge na katika kipindi chake cha uongozi alihudumu kwa vipindi viwili.

“Kwa mwaka huu 2021 itakuwa ni maadhimisho ya 17 kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine toka kumbukizi ya kwanza mnamo mwaka 1992  ya maadhimisho hayo  ambayo hufanyika kila mwaka Chuoni ” alisema prof. Mwatawala.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kumbukizi ya hayati Edward Sokoine Moringe Prof. Samweli Kabote kutoka SUA alisema kuwa huwezi kuongea historiaya Chuo cha Sokoine cha Kilimo SUA bila kumtaja Hayati Sokoine kwasababu Chuo kimebeba jina lake.

 Wiki ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo, Teknolojia za kilimo, kuzalisha kwa tija na ushindani katika Soko, Kuelekea Nchi ya Uchumi wa juu wa Kati.   

No comments:

Post a Comment

Pages