HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 17, 2021

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar awata wauumini kuendeleza Ibada baada ya kumalizika kwa Mwezi Ramadhani

 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla Akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kukamilika kwa Ibada ya Sala ya Ijuma kwenye Msikiti Jeshi Jang’ombe.

Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakifuatilia nasaha za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed mara baada ya kukamilika kwa Ibada ya Sala ya Ijuma kwenye Msikiti Jeshi Jang’ombe Mjini Zanzibar.

Picha na – OMPR – ZNZ.

                                              

 

NA MWANDISHI WETU

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alisema Fadhila za utukufu wa Mwezi wa Ramadhani zinaeleweka na Waumini waliowengi na kinachohitaji kwao kuendeleza Ibada hata baada ya kumalizika kwa Mwezi huo.

Akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kukamilika kwa Ibada ya Sala ya Ijuma kwenye Msikiti Jeshi Jang’ombe Mheshimiwa Hemed Suleiman alieleza kwamba mshikano. 

Alisema wapo baadhi ya Waumini wamekuwa na tabia ya kufanya Ibada kwenye Mwezi wa Ramadhan pekee jambo ambalo linakwenda kinyume na ucha mungu unaopaswa kutekelezwa muda wote wa maisha ya Muumini.

Mheshimiwa Hemed aliendelea kuwakumbusha waumini hao kuwa, mwezi wa ramadhani ni kipindi cha  kusaidiana, kwa  kuzidisha utoaji wa sadaka na kuwaasa wenye tabia ya kurimbikiza vyakula hadi kuvimwaga, hali ya kuwa wapo wenzao, ambao hawana cha kukila.

Akigusia suala la bei za bidhaa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema serikali imekuwa ikisamehe ushuru kwa bidhaa za vyakula ili kuwasaidia wananchi kumudu futari, lakini inasikitisha kuona baadhi yao hupandisha bei za bidhaa jambo ambalo linawakwaza wananchi kupata huduma hiyo.

Aidha alitanabahisha kwamba baadhi ya Wafanyabiashara wanashindwa kuwa na uchungu Kwa Wananchi wanaowahudumia na badala yake wanaufanya mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuwa ni chumo kubwa la kupata faida iliyonona tabia ambayo inastahiki kuondoshwa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba Wananchi Mitaani pale wanapoona uzembe  wa makusudi ni vyema wakatoa taarifa mapema katika ngazi iliyo karibu nayo na baadae itaifikisha katika ngazi husika.

Mapema akitoa Hotuba katika sala ya Ijumaa MaalimMashi Yussuf Mashi aliwakumbusha wale walioamini kuendelea kufunga Mwenzi Mtukufu wa Ramadhan na kinyume chake ni kuukataa Uislamu jambo ambalo dhambi isiyosameheka.

Maalim Mashi Yussuf  aliwaeleza Waumini hao kwamba lazima wazingatie taratibu za Ibada katika kujiepusha na vitimbi vya Shetani kwa kusoma sana Kitabu Kitakatifu cha Quran ibada itayokwenda sambamba na kuzidisha sala za Usiku.

Alisema hatua hiyo ndio njia pekee kwa Kila Muumini atakayejikita kwa hayo atafanikiwa kumshinda shetani na tayari atajikaribisha kwa Muumba wake katika utekelezaji wake wa ucha Mungu.

 

No comments:

Post a Comment

Pages