HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 13, 2021

TIOB YAZINDUA KITAMBULISHO KIPYA CHA KIDIGITALI CHA WANACHAMA


Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitambulisho kipya cha cha kidigitali cha wanachama wa TIOB, Kushoto ni Farid Seif Mkuu wa Kitengo cha Kadi Benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Msusa, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kitambulisho kipya cha cha kidigitali cha wanachama wa TIOB. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kadi Benki ya CRDB, Farid Seif na Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa.
Baadhi ya wadau walioshiriki uzinduzi huo.


Wadau.

Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Taasisi ya TIOB leo Aprili 13, 2021 wamezindua kitambulisho kipya cha kidigitali cha uwanachama wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TIOB, Patrick Mususa, wamezindua rasmi Kadi mpya ya Kitambulisho cha uwanachama wa TIOB.


Uzinduzi wa Kitambulisho hiki umewezeshwa na CRDB Bank PLC, mmoja wa wanachama wa taasisi ya TIOB na vile vile mdau mkuu katika kujenga taaluma na uelewa wa watoaji na walaji huduma za kifedha nchini ikiwa ni pamoja na walioajiriwa katika benki hiyo, mawakala na wateja wa benki hiyo.

Wanachama wa TIOB wataweza kufaidi huduma hii mpya ya kupatiwa kitambulisho cha uwanachama kipya cha kidigitali na chenye uwezo wa kuhifadhi fedha na vile vile kukamilisha miamala ya kifedha na hivyo kupunguza adha mbali mbali za malipo kwa ajili ya huduma zinazopatikana TIOB na kwingineko. 

Muhimu zaidi, kitambulisho hiki itakuwa ni ufunguo kwa wanachama wa TIOB ambao wengi wao wana malengo ya kuwa wataalamu wa kifedha, kwani itawapa fursa ya kwanza kabisa ya kutumia mbinu mpya ya kidigitali kwa ajili ya kukamilisha miamala ya kifedha kupitia kadi. 

 

Vile vile kitambulisho hiki kitawapatia wanachama wote wa TIOB punguzo Ia gharama katika maduka maalum ya bidhaa na huduma nje ya TIOB na hivyo kuchangia katika kuboresha zaidi matumizi ya fedha ya wanachama wake.

Kitambulisho hiki kipya cha uwanachama kitadumu kwa kipindi cha miaka mitano (5) baada ya kupewa mwanachama. Vilevile, Kitambulisho kipya cha uwanachama wa TIOB kitampa mwanachama utambulisho uliohakikiwa na takwimu zake kuboreshwa. Pia kitambulisho hiki kitamuwezesha mwanachama kufanya malipo ya huduma mbali mbali zinazopatikana TIOB.

Vile vile, Kitambulisho hiki kipya cha uwanachama wa TIOB kuanzia sasa itatumika kama mfumo mpya wa utambulisho katika oflsi na huduma mbali mbali za TIOB ikiwemo usajili na ushiriki katika mitihani ya kitaaluma iliyoandaliwa na TIOB; matumizi ya huduma za maktaba za TIOB na huduma zingine zote za wanachama. Kitambulisho hiki kipya cha kidigitali kitakuwa kitambulisho rasmi cha mwanachama wa TIOB na kitatumika badala ya kadi 2a uanachama za awali.

No comments:

Post a Comment

Pages