Meneja Mwandamizi wa Huduma za Ziada za Benki ya CRDB Ndugu Mangire Kibada akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma. |
Kongamano hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya uvumbuzi “Innovation Week” ambayo yataambatana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliasisiwa mwaka 2019 kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Akizungumza katika kongamano hilo, Meneja Mwandamizi wa Huduma za Ziada za Benki ya CRDB, Mangire Kibada amaesema kuwa Benki ya CRDB imeamua kudhamini wiki ya uvumbuzi kwa kuwa inaamini katika kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja ambazo zinapatikana kwa njia ya kuwekeza katika uvumbuzi.
“Kwetu Benki ya CRDB tunaamini uvumbuzi ni kitu pekee ambacho kinaweza kututofautisha na wengine katika soko na hivyo kuifanya benki yetu kuendelea kuwa kinara sokoni kwa kuweza kutimiza mahitaji ya wateja wa makundi mbalimbali” alisema Kibanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuainisha na kupendekeza hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika kutengeneza na kutekeleza mipango ya uvumbuzi katika sekta ya fedha.
No comments:
Post a Comment