Mkurugenzi
wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul – Razaq Badru na
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala na Usajili, Ufilisi na Udhamini
(RITA) Bi. Emmy Hudson akimkabidhiana mkataba mara baada ya kusaini makubaliano ya kimkakati ya kufanya kazi.
Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul – Razaq Badru akifafanua jambo katika mkutano na waandishi (hawapo pichani)jijini Dar es Salaam.
Dar es salaam:
Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini (RITA) wameingia makubaliano ya kufanya kazi kwa ushirikiano
ikiwemo kuhakiki vyeti vya kuzaliwa na vifo kwa waombaji mikopo ya elimu
ya juu na kubadilishana taarifa
Akizungumza
jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul – Razaq
Badru, alisema lengo la makubaliano yao ni kuhakikisha wanafanya kazi
kwa ufanisi ikiwemo kuepuka wanafunzi kuleta taarifa zilizoghushiwa.
Bw.
Badru alisema kupitia makubaliano hayo yana tija kwa pande zote mbili
HESLS na RITA kwani wamekuwa wakishirikiana hata bila hati inayosainiwa.
“Tutabadilishana
uzoefu wa kiutendaji kati ya watumishi ili kuhakikisha kila jambo
linafanyika kwa ufanisi mkubwa” alisema Bw. Badru.
Bw. Badru aliongeza kuwa Juni 25 mwaka huu wanatarajia kutoa mwongozo wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2021/2022.
Alisema mwongozo huo ambao utapatikana katika lugha ya kiswahili na kiingereza katika tovuti ya HESLB – www.heslb.go.tz,
na kuwataka wanafunzi kusoma kwa makini na ukizingatia kabla ya kuanza
kuomba pale dirisha au mfumo utakapofunguliwa kwa miezi miwili kuanzia
mwezi Julai 1 mwaka huu.
"Tupo
katika maandalizi ya kwenda mikoa mbalimbali na kambi za Jeshi la
kujenga Taifa (JKT) kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi wanatarajia
kuomba mkopo wa elimu ya juu".
Alisema
tayari bunge limeidhinisha bajeti ya Shillingi bilioni 500 kwa ajili ya
mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2021/2022 inayotarajia kuwanufaisha
wanafunzi takribani 160,000.
"katika
utoaji wa mikopo jumla wanafunzi 149, 472 wamepangiwa mikopo yenye
thamani ya Shillingi bilioni 464 kati ya hizo tayari serikali imeshatoa
asilimia 85 ya bajeti yote"
Aidha
pia ameelezea hatua ambazo bodi imekuwa ikizichukua katika ukusanyaji
wa mikopo mpaka sasa wamekusanya Shillingi bilioni 168 ambapo ni sawa na
asilimia 88.4 , huku akieleza kuwa lengo ni kukusanya bilioni 190
katika mwaka wa fedha 2020/ 2021.
Kwa
upande wake kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala na Usajili, Ufilisi na
Udhamini (RITA) Bi. Emmy Hudson, amewataka wanafunzi wote kutuma maombi
yao kwa wakati, huku taarifa zao zikiwa katika mfumo wa PDF.
Alisema
kila mwaka kumekuwepo na changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi kuwa na
utamaduni kwa uchelewa kutuma maombi, hivyo amewataka kuhakikisha kila
kitu kinafanyika kwa wakati ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.
“Tutaendelea
kufanya kazi kwa kushiriki na ufanisi ili kila kitu kiende sawa katika
kuhakikisha taarifa zinakuwa sahihi kwa waombaji wa mikopo ya elimu ya
juu” amesema Bi. Hudson
No comments:
Post a Comment