HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 14, 2021

HESLB, RITA Wasaini Makubaliano Ya kimkakati Kuongeza Ufanisi


 
Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul – Razaq Badru na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala na Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bi. Emmy Hudson akimkabidhiana mkataba mara baada ya kusaini makubaliano ya kimkakati ya kufanya kazi.

 Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul – Razaq Badru akifafanua jambo katika mkutano na waandishi (hawapo pichani)jijini Dar es Salaam.
 
Dar es salaam:
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) wameingia makubaliano ya kufanya kazi kwa ushirikiano ikiwemo kuhakiki vyeti vya kuzaliwa na vifo kwa waombaji mikopo ya elimu ya juu na kubadilishana taarifa

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul – Razaq Badru, alisema lengo la makubaliano yao ni kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi ikiwemo kuepuka wanafunzi kuleta taarifa zilizoghushiwa.

Bw. Badru alisema kupitia makubaliano hayo yana tija kwa pande zote mbili HESLS na RITA kwani wamekuwa wakishirikiana hata bila hati inayosainiwa.

“Tutabadilishana uzoefu wa kiutendaji kati ya watumishi ili kuhakikisha kila jambo linafanyika kwa ufanisi mkubwa” alisema Bw. Badru.

Bw. Badru aliongeza kuwa Juni 25 mwaka huu wanatarajia kutoa mwongozo wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2021/2022.

Alisema mwongozo huo ambao utapatikana katika lugha ya kiswahili na kiingereza katika tovuti ya HESLB – www.heslb.go.tz, na kuwataka wanafunzi kusoma kwa makini na ukizingatia kabla ya kuanza kuomba pale dirisha au mfumo utakapofunguliwa kwa miezi miwili kuanzia mwezi Julai 1 mwaka huu.

"Tupo katika maandalizi ya kwenda mikoa mbalimbali na kambi za Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi wanatarajia kuomba mkopo wa elimu ya juu".

Alisema tayari bunge limeidhinisha bajeti ya Shillingi bilioni 500 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2021/2022 inayotarajia kuwanufaisha wanafunzi takribani 160,000.

"katika utoaji wa mikopo jumla wanafunzi 149, 472 wamepangiwa mikopo yenye thamani ya Shillingi bilioni 464 kati ya hizo tayari serikali imeshatoa asilimia 85 ya bajeti yote"

Aidha pia ameelezea hatua ambazo bodi imekuwa ikizichukua katika ukusanyaji wa mikopo mpaka sasa wamekusanya Shillingi bilioni 168 ambapo ni sawa na asilimia 88.4 , huku akieleza kuwa lengo ni kukusanya bilioni 190 katika mwaka wa fedha 2020/ 2021.

Kwa upande wake kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala na Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bi. Emmy Hudson, amewataka wanafunzi wote kutuma maombi yao kwa wakati, huku taarifa zao zikiwa katika mfumo wa PDF.

Alisema kila mwaka kumekuwepo na changamoto kubwa kwa  wanafunzi wengi kuwa na utamaduni kwa uchelewa kutuma maombi, hivyo amewataka kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa wakati ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

“Tutaendelea kufanya kazi kwa kushiriki na ufanisi ili kila kitu kiende sawa katika kuhakikisha taarifa zinakuwa sahihi kwa waombaji wa mikopo ya elimu ya juu” amesema Bi. Hudson
 
 

No comments:

Post a Comment

Pages