Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeiry, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao kilichowakutanisha viongozi wa dini kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kujenga undugu kati ya waamini wa dini zote.
Viongozi
wa Dini nchini wameiomba Serikali na Mamlaka husika kuharakisha
mchakato wa ushughulikiaji na usikilizaji wa kesi za viongozi wa dini ya
Kiislamu walioko magerezani kwa miaka mingi ili haki itendeke na kwamba
watakaokutwa na hatia wachukuliwe hatua za kisheria.
Ombi
hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Abubakar Bin Zubeiry baada ya Kikao kilichowakutanisha viongozi hao
kumaliza kikao kilichojadili masuala mbalimbali ikiwemo kujenga undugu
kati ya waamini wa dini zote, mustakabali wa taifa na kuhamasisha
kudumisha amani, umoja na mshikamano.
Amesema
kuwa anaiomba mahakama na MKurugenzi wa Mashtaka na Serikali kwa ujumla
kuharakisha usikilizaji wa kesi wa viongozi wa dini kwani wameshikiliwa
kwa muda mrefu bila kujua hatma zao.
"
Tunaiomba mahakama, DPP na Serikali itatue kesi zikilizwe kwa haraka
watakaokutwa na makosa wachukuliwe hatua za kisheria," amesema Mufti Bin
Zubeiry.
Amebainisha kuwa viongozi wa dini
wanaoshikiliwa na vyombo vya sheria watendewe haki kwa kusikilizwa kesi
zao kwani kuwaweka ndani muda mrefu ni kuwanyima haki zao za msingi.
Kwa
upande wake Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania,
Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa amesema ili
kukakikisha linakuwa na kizazi chenye maadili mema yatakayochangia
maendeleo ya taifa na kwamba kila mzazi anatakiwa kutimiza wajibu wake
kwa kuwapa watoto wao malezi mema.
Askofu Dkt.
Malasusa amesema kila dini inassisitiza na kuhimiza kila mwenye mtoto
kutoa malezi bora yanayochangia ustawi wa jamii imara na taifa lenye
maendeleo.
Amewasisitiza na kuwahimiza viongozi
wa madhehebu yote kuendelea kuwahamasisha waamini wao kudumisha umoja,
amani na mshikamano uliopo.
Mufti huyo amesema
hadi sasa Baraza la Waislamu Tanzania halijapata taarifa sahihi za watu
wanaotaka kwenda Hijja kutoka Wizara ya Hijja ya Saudia Arabia na
Ubalozi wa nchi hiyo nchini hivyo zikilifikia watatoa taarifa.
Naye
Askofu wa Kanisa la Menonite Tanzania, Dayosisi ya Masahariki na Pwani,
Nelson Kisare amesema waamini wa dini wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa
kuendelea kuilinda nchi hata baada ya kifo cha Rais Dkt. John Magufuli
hivyo ni kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni jambo jema na la
kihistoria kwa taifa.
Aidha, amesema jamii
inatakiwa kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto kwani ni dhambi na
kusisitiza elimu kutolewa kwa wahusika ili watambue madhara ya kukiuka
haki za kundi hilo.
Askofu Mkuu wa Elimu ya
Pentekoste Peter Konki amekemea vitendo viovu ya kudhihaki Marais
wastaafu na aliyeoko madarakani kwa lugha ya matusi kwani kufanya hivyo
kuwakosea kulikosea taifa kwa ujumla.
Ameiomba
Serikali kushughulikia suala la mfumuko wa bei kwani linaathiri maisha
ya watu wa hali ya chini kwani wengi hushindwa kumudu gharama za maisha.
No comments:
Post a Comment