Waziri wa Elimu ya Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha
Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania, lililofanyika Juni 9,
2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua rasmi Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha
Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania, lililofanyika Juni 9,
2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua rasmi Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha
Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania, lililofanyika Juni 9,
2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo iliyotolewa kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza Elimu ya Watu Wazima. Dk. Akwilapo alipokea kwa niaba ya familia ya Mwalimu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo iliyotolewa kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza Elimu ya Watu Wazima. Dk. Akwilapo alipokea kwa niaba ya familia ya Mwalimu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa tuzo za Shahada za Umahiri katika Mchango wa kuendeleza Elimu ya Watu Wazima Tanzania, Mkuu wa Taasisi hiyo, Dk. Michael Ng'umbi kwa kutambua mchango wa
taasisi hiyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha
Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania, lililofanyika Juni 9,
2021.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu
ya Watu Wazima Tanzania, Dk. Michael Ng'umbi wakati wa ufunguzi wa Kongamano wa
Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima
Tanzania, lililofanyika leo Juni 9, 2021 mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu ya Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akitoa ufafanuzi kwa waziri mkuu wakati alipotembelea banda la Taasisi ya Elimu Tanzania.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Serikali
imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafufua
madarasa ya Elimu ya Watu Wazima (MEMKWA) pamoja na kutenga fedha za
kuwalipa walimu wanaofundisha madarasa hayo lengo likiwa kuendelea
kupunguza kundi la watu wasio jua kusoma na kuandika pamoja na
kuwaongezea ujuzi unaoendana na mazingira yao.
Aidha,
imewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote kufanya kampeni ya kutoa
hamasa itakatayosaidia watu kujitokeza kupatiwa elimu katika maeneo
yaliyotengwa kutolea elimu hiyo.
Maagizo hayo
yametolewa jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika
Ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya
Watu Wazima Tanzania lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) kupitia Shule Kuu ya Elimu ya chuo hicho.
Amesema
kuwa kuna maeneo ambayo madarasa ya kutolea elimu yamekufa hivyo na
juhudi za dhati zinatakiwa kufanywa na wakaurugenzi kuyarudisha na
kuwahimiza watu waliokosa fursa ya kupata elimu kuhudhuria.
"
Wakurugenzi wote wayafufue madarasa ya MEMKWA katika maeneo ambayo
hakuna vile watenge fedha za kulipa walimu tunafanya kuendeleza juhudi
kupunguza ujinga wa kutojua kusoma na kuandika," amesema Majaliwa.
Ameiagiza
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na UDSM kufanya tafiti kuhusu takwimu
halisi za idadi ya watu waliofaidika na elimu hiyo, wasionufaika pamoja
na kuja na njia za kukabiliana na changamoto zinazoikabili elimu hiyo.
Maagizo
mengine ni Wizara ya Elimu ya Sayansi na Teknolojia kusimamia misingi
ya kuanzishwa taasisi hiyo kwa kuhkikisha inapunguza idadi ya watu
wajinga,taasisi ya elimu hiyo kuandaa mkakati wa kuifikisha maeneo ya
vijijini sio mijini tu, kuimarisha mfumo thabiti kwa wanakisomo kwa kila
mwaka kwa kuimarisha programu, mitihani na utoaji vyeti kwa wahitimu.
Waziri
wa wizara hiyo Profesa Joyce Ndalichako amesema maadhimisho yanafanyika
kuendeleza mchango wa elimu hiyo kwa taifa tanngu ilipotangazwa mwaka
1970.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Leonard
Akwilapo amesema utaoji wa elimu hiyo ni mwendelezo wa kutekeleza lengo
la nne ya Malengo ya Millenia ya kuhakikisha jamii inapata elimu
jumuishi.
Kwa upande wake Amidi Mkuu wa Shule
hiyo Daktari Kafanabo amesema kongamano hilo linaenzi mchango Hayati
Mwalimu Julius Nyerere katika kuikomboa nchi katika maradhi ya ujinga,
umaskini na maradhi kupitia elimu hiyo.
Dkt.
Kafanabo amesema kongamano litaangalia wapi elimu hiyo ilipotoka na
inapokwenda na kusisitiza kuwa mawasilisho mbalimbali yatatolewa na
watalaam wa taasisi mbalimbali.
Naye Makamu
Mkuu wa Chuo hicho Profesa William Anangisye amesema uhai wa chuo upo
kwenye tafiti na kwamba kongamano hilo limeandaliwa ili kufanya tathmini
ya elimu hiyo ilipofikia na inapoelekea.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,
Kisare Makori amesema amempongeza waziri Majaliwa na kusema kongamano
hilo litaibua mawazo yatakayosaidia kukabiliana na ujinga.
Mkurugenzi
wa Taasisi hiyo Michael Mumbi amesema kazi yao ni kusanifu vijana na
watu wazima wasio jua kusoma na kuandika kupata ustadi na kuwaondolea
ujinga.
Katika kongamano hilo Tuzo za
Shahada za Umahiri katika Mchango wa kuendeleza elimu hiyo zilitolewa
ikiwemo ya Mwalimu Nyerere kwa mchango wake katika kupinga ujinga
kupitia elimu hiyo, tuzo nyingine ilitolewa kwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima pamoja na wadau mbalimbali.
No comments:
Post a Comment