HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 15, 2021

CRDB Bank International Marathon yanoga Dar


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akivishwa medali na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay, wakati wa mbio za CRDB Bank Marathon 2021 zilizofanyika leo Agosti 15 Jijiji Dar es Salaam, ambapo waziri Mkuu alikimbia kilometa 5. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
  

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakikabidhi kwa pamoja mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 200 kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi, kwa ajili ya kusaidia watoto wanaopata matibabu katika taasisi hiyo. Fedha hizo zimetokana na mbio za CRDB Bank Marathon zilizofanyika Jijiji Dar es Salaam leo Agosti 15, 2021.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakikabidhi kwa pamoja mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 104 kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel (wa pili kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselege (wa tatu kulia) kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Mawasiliano katika taasisi hiyo.

Waziri Mkuu akishiriki mbio za CRDB Bank Marathon kilometa 5.
Waziri Mkuu akiongoza mbio za CRDB Bank Marathon kilometa 5.
Washiriki wa CRDB Bank Marathon wakichuana katika  mbio za kilometa 42 na 21.

Washiriki wa mbio za kilometa 10 wakichuana.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa CRDB Bank Marathon kilometa 21 kwa upande wa wanawake, Pouline Eskon kutoka Kenya.
Angel John kutoka Tanzania akipokea zawadi ya mshindi wa tatu kilometa 42 kwa upande wa wanawake kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza kilometa 42 kwa upande wa wanawake, Selmith Muriykh.
Paul Eyanae kutoka Kenya akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza kilometa 42.
Paulo Festo Ikungu kutoka Tanzania akipokea zawadi ya mshindi wa tatu kilometa 42. 
 

NA TULLO CHAMBO

MBIO za kimataifa za CRDB Bank zimefanyika kwa mafanikio kwenye viwanja vya Green jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa wanariadha kutoka Kenya wakitamba.


Katika mbio hizo ambazo Mgeni Rasmi alikuwa Waziriki Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, ikishuhudiwa katika Kilomita 42 kwa wanaume mshindi akiibuka Paul Eyanae kutoka akitumia saa 2:15.27 akifuatiwa na Agustino Sulle kutoka Talent Club ya Arusha saa 2:15.47 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Paulo Festo wa Singida 2:15.56 wakati nafasi ya ikachukuliwa na Rashid Muna pia wa Singida 3:18.12.


Kwa upande wa wanawake Kilomita 42, mshindi akiibuka Selmith Muriuki aliyetumia saa 2:42.02 akifuatiwa na Isgah Cheruto 2:46.04 wote kutoka Kenya watatu Angel John wa Arusha 2:46.04 wakati mshindi wa nne akiwa Ni Yulita Tanui wa Kenya saa 3:00.58.


Kilomita 21 wanaume, Panuel Mkungo kutoka Kenya akiibuka kidedea akitumia sàa 1: 03.29 akifuatiwa na Emmanuel Giniki wa Arusha saa 1:03.31 nafasi ya tatu Faraja Lazaro pia Arusha 1:03.48 huku nafasi ya nne ikienda kwa Abel Chebet kutoka Uganda 1:03.49.


Upande wa Kilomita 21 wanawake kinara akiibuka Pouline Eskon akifuatiwa na Cynthia Kosgei huku nafasi ya tatu ikienda kwa Lilian Jepkemboi wote kutoka Kenya huku nne bora ikifungwa na Grace Jackson wa JKT Arusha.


Kwenye Mbio za Kilomita 10 wanawake mshindi  alikuwa ni Transfora Musa wa JKT Arusha akifuatiwa na Anastasia Doromondo Arusha, Cecilia Ginoka wa JWTZ Arusha  nafasi ya tatu huku ya nne ikienda kwa Tunu Andrea wa Singida.


Kilomita 10 wanaume mshindi ni Joseph Panga  JWTZ Arusha, akifuatiwa na Kaposhi Laizer wa Arusha, nafasi ya tatu Inyasi Sulle pia wa Arusha huku mshindi wa nne akiwa Ni Nelson Priva kutoka JKU Zanzibar.


Pia CRDB Bank International Marathon ilikuwa na mbio za Km 5 Fun Run sambamba na mbio za Baiskeli ambapo    Mrembo wa Miss Tourism Njombe, Zawadi Mwambi aliendelea kuonyesha umahiri akishika nafasi ya nne ikiwa ni wiki chache toka aliipoibuka kidedea katika Tamasha la Majimaji Selebuka lililofanyika mjini Songea mkoani Ruvuma.


Kufanyika kwa mafanikio  CRDB Bank International Marathon, kunazidi kuongeza chachu ya mchezo wa Riadha Tanzania ambapo Hadi sasa kunaongezeka idadi ya Mbio za Kimataifa, ambapo nyingine Ni NBC Dodoma International Marathon na Kilimanjaro Marathon.

No comments:

Post a Comment

Pages