HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 12, 2021

Kamisaa Anne Makinda awasisitiza wadau kuihamasisha na kuielimisha jamii umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi


Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi wa Tanzania Bara ambaye pia ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda. 

 Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

 

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi wa Tanzania Bara ambaye pia ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda amewasisitiza Wadau washiriki wa  Mkutano wa kujadili Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Mwezi Agosti mwakani kutoa maoni na mapendekezo yatakayochangia uboreshaji wa mkakati huo pamoja na kuituma fursa hiyo kuipa jamii uelewa na umuhimu wa sensa hiyo kitaifa.

Msisiitizo huo ameutoa leo jjijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano huo ulioshirikisha  wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari, wahariri wa vyombo vya habari, Jukwaa la Habari Tanzania (TEF), taasisi za kitakwimu, Viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) pamoja na wa Ofisi Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar (OCGS).

Amesema kuwa Tanzania ina watu zaidi ya milioni 60 na kwamba wadau washiriki wanatakiwa kutambua umuhimu kwa taifa kwa kuwa wazalendo baada kuchangia maboresho ya mkakati huo kwenda kuelimisha jamii umuhimu wa sensa hiyo itakayofanyika nchi nzima.

" Nwawaomba mtumie usukani huu kwenda kutoa elimu kwa jamii juu umuhimu wa sensa baada ya majadiliano kila mshiriki mdau awe mzalendo ajitoe kwenye kuelimisha na kuboresha mkakati huo," amesema Kamisaa Makinda.

Amebainisha kuwa kila baada ya miaka 10 nchi hufanya sensa hiyo ambapo idadi ya watu huhesabiwa kwa kuuliza maswali sawa kwa kila mwananchi na kwamba huisaidia Serikali kupata taarifa muhimu za kupanga maendeleo inayoendana na jamii pamoja na kuzisaidia Serikali za Mitaa, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kupima na kutekeleza mipango hiyo.

Amessisitiza kuwa senya ya mwaka 2022 itaegemea  kuuliza maswali katika vipengele mbalimbali vikwemo vya umri, jinsi, ndoa, uraia, uhamiaji, vitabulisho vya taifa, uhai wa wazazi, vifo vya uzazi kwa wanawake na hali ya ajira.

Vingine ni hali ya elimu, umiliki wa ardhi, udhibiti wa Mazingira, taarifa za kilimo, misitu, Mfufo wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) pamoja na umiliki wa majengo.

Ameongeza kuwa sensa ya mwakani itakuwa sensa ya sita tangu kuundwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzyika kufanyika na kwamba sensa ya majaribio itafnyika mwishoni mwa mwezi wa Agosti mwaka huu.

Amefafanua kuwa dhamira ya Serikali zote ni kufanya sensa iliyo bora  tofauti na zilizopita kwani itafanywa kwa kutumia matumizi ya Tehama yatakayosaidia kupungua gharama, kuokoa muda,makosa ya kibinadamu na utoaji takwimu sahihi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu za Kijamii kutoka OCGS, Khadija Khamis amesema wanatarajia kufanya sensa kwa kuwa katika mchakato wa kuboresha mkakati huo wameshirkisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, Serikali, na sasi za kiraia huku akiongeza sensa ya majaribio visiwani humo itafanyika mwishoni mwamwezi huu katika wilaya 10.

Aidha, amesema sensa ya watu na makazi hutumika kupima na kupanga maendeleo ya jamii, sera, ajira na mahitaji ya makundi mbalimbali kulingana kufuatana na jinsi pamoja na umri.

Naye Meneja Ofisi ya NBS wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Kapala amesema kwa kushirikiana na wadau hao wapo katika mkakati kabambe wa kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kutosha kabla ya kufanyika sensa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages