Kiongozi
wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi akipanda
mti wa mkorosho katika shamba linalomilikiwa na Kikosi Cha Ruvu JKT.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha akipanda mti katika shamba Hilo katika mradi wa mikorosho ambao ulipitiwa na mbio za Mwenge wa uhuru.
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Kiongozi
wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi amewataka
vijana kubadilika kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali mbali mbali
ikiwemo kilimo ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipokwenda kutembelea na kukagua shamba la mikorosho samba na kupanda miti.
Aliongeza
kuwa kwa Sasa sekta ya kilimo inasaidia kwa kiasi kikubwa katika
kuwasaidia vijana kuondokana na umasikini kupitia fursa mbali mbali za
ajira.
Aidha alifafanua
kwamba endapo vijana wakajikita zaidi katika kujishugulisha na kilimo
Cha mikorosho kutaweza kuwaongezea zaidi kujiongezea kipato.
Mbali
na kutembelea mradi huo wa kilimo Cha mikorosho alikwenda kutembelea
katika kituo Cha afya mlandizi na kunionea jinsi ya mfumo wa Tehama
unavyofanya kazi na kuwaagiza watendaji kuhakikisha wanasimia vizuri
ukusanyaji wa mapato.
Kadhalika
akielezea juu ya mapambano dhidi ya marelia alisema kuwa ni vema
wataalamu wa afya wakaweka mipango madhubuti ambayo itasaidia kupungua
kasi ya maambukizi hayo.
Awali
mkuu wa wilaya ya Kibaha ambaye aliupokea mwenge huo kutoka kwa mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo alibainisha kuwa miradi 13 itatembelewa.
Pia alisema kuwa miradi yote hiyo imegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni 2 ambayo itakuwa katika sekta mbali mbali.
Caption
.1 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Luteni Josephine
Mwambashi akipanda mti wa mkorosho katika shamba linalomilikiwa na
Kikosi Cha Ruvu JKT.
Caption
2.Mkuu wa Wilaya ya Kibaha akipanda mti katika shamba Hilo katika mradi
wa mikorosho ambao ulipitiwa na mbio za Mwenge wa uhuru.
No comments:
Post a Comment