Dar es Salaam, Tanzania
MCHAMBUZI mahiri wa soka nchini, Alex Theogenis Kashasha 'Mwalimu Kashasha', amefariki dunia leo Alhamisi Agosti 19, wakati akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Kairuki, Iliyopo Mikocheni jijini Dar wa Salaam.
Mwalimu Kashasha alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na aina yake ya uchambuzi, uliojaa ufundi na mbinu, akivuta hisia za wengi miongoni mwa wasikilizaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), alikokuwa akifanya kazi TBC1, TBC Taifa, TBC FM na vyombo vingine alivyoalikwa kufanya chambuzi.
Hata hivyo, taarifa za kifo chake hazijaeleza Mwalimu Kashasha alikuwa akisumbuliwa na maradhi gani yaliyomlaza Hospitali kwa matibabu, kiasi cha kusababisha kifo chake.
Habari Mseto itaendelea kukuletea taarifa mbalimbali kuhusu kifo na mazishi ya Marehemu Mwalimu Kashasha.
Bwana Ametoa
Bwana Ametwaa
Jina la Bwana Lihimidiwe.
No comments:
Post a Comment