Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 23, 2021.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa imekamilisha Awamu ya Kwanza ya
Udahili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza ya Taasisi za Elimu ya Juu kwa
mwaka wa masomo wa 2021/22 huku ikibainisha katika awamu hiyo jumla ya
waombaji 68,019 sawa na asilimia 73.2% ya waombaji wote wamepata
udahili vyuoni.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar
es Salaam na Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Charles Kihampa wakati
akizungumza na wanahabari kuhusu kukamilka kwa awamu ya kwanza ya
udahili na kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili wa shahada hiyo kwa
mwaka wa masomo huo utakaoanza rasmi Agosti 24 hadi Septemba 6 mwaka
huu.
Amesema kuwa katika awamu ya kwanza jumla
ya waombaji 92,809 walituma maombi ya kujiunga katika vyuo 74
vilivyoidhishwa kudahili na kwamba jumla ya proramu 724 zimeruhusiwa
kudahili ukilinganishwa na programu 686 za mwaka wa maomo wa 2020/21.
Amebainisha
kuwa kwa upande za nafasi za mwaka huu wa masomo kuna jumla ya nafasi
164,901 ikilinganuishwa na nafasi 157,770 za mwaka uliopita na
kusisitiza ni ongezeko la la nafasi 7,131 sawa na asilimia 4.5 katika
progamu za shahada ya kwanza.
" Mwenendo wa
udahili wa wamau ya kwanza kwa kpindi cha miaka minne (2018/2019 hadi
2021/22 inaonesha ongezeko kubwa la waombaji ikiashiria ongezeko la
wahitimu wa Kidato cha Sita na wale wa Stashahada," amesema Profesa
Kihampa.
Amewasisitiza waombaji ambao
hawakuweza kutuma maombai ya udahili ua kudahiliwa katika awamu ya
kwanza kutokana na sababu mbalimbali watumie fursa fursa ya awamu ya
pili kutuma maombi kwenye vyuo wanavyovipenda kwani taasisi za elimu
hiyo zimeshaelekezwa kutangaza progamu ambazo bado zina nafasi.
Pia,
amewahimiza waomabji wa vyuo kuzingatia utaratibu wa udahili kwa
awamuya pili kama inavyoelekezwa kwenye kalenda ya udahili iliyoko
kwenye tovuti ya tume hiyo
Aidha, Prof. Kihampa
ametoa wito waombaji udahili wa shahada ya kwanza kwa kuwakumbusha
masuala yote yanayohusu udahili au ya kujithibisha katika chuo kimoja
wayawasilishe moja kwa moja kwenye vyuo husika na kwamba watakaopta
changamoto kwenye uthibitisho vyuo vimshaelekezwa kupokea taarifa zao na
kuzitafutia ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu
zilizowekwa.
Amewaasa wananchi kuepuka
kupotoshwa na watu wanaojita mawakala au washauri wakijifana kutoa
huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini na
kuwahimiza waombaji waliodahiliwa katika zaidi ya chuo kimoja
kuthibitisha udahili wao kwenye chuo kimojawapo kuanza kesho hadi
Septemba 6 mwaka huu kwa namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe
mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa
kuomba udahili.
No comments:
Post a Comment