Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa akizungumza na waandishi
wa habari hawapo pichani kuhusiana na matukio mbali mbali ikiwemo ya
watu watatu kupoteza maisha.
NA VICTOR MASANGU, PWANI
WATU watatu wamefariki dunia
kikatili katika matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Pwani ,ikiwa ni
pamoja na mwanamke kubakwa hadi kifo na mwanamke mwingine kukatwa na
kitu chenye ncha kali shingoni na kutenganishwa na kiwiliwili.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Pwani,Wankyo Nyigesa alisema tukio la kwanza lilitokea Agosti 8, mwaka
huu katika Kitongoji cha Tobora Kata ya Msata ambapo mwanamke mmoja (26)
Mzigua, Mkazi wa Pongwe Msungura alibakwa kisha kuuawa.
Mwanamke
huyu mwili wake ulitelekezwa vichakani, licha ya mtuhumiwa mmoja
amekamatwa kuhusiana na tukio hilo na Jeshi la Polisi linaendelea
kumhoji.
Katika tukio jingine Kamanda
Nyigesa,alisema mwanamke mwingine ambaye jina lake limehifadhiwa Mkazi
wa Kijiji cha Kitonga Wilayani Bagamoyo aliuawa kwa kukatwa na kitu
chenye ncha kali shingoni kisha kutenganisha kichwa na kiwiliwili.
Nyigesa,alisema
kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 4 mwaka huu saa 12 jioni huko katika
Kijiji cha Kitonga ambapo marehemu alivamiwa shambani kwake na watu
wasiojulikana na hivyo kutekeleza mauaji hayo.
Pamoja
na hayo ,mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Kwarohombo Kata ya Mbwewe
Chalinze ambaye jina lake halijafahamika aliuawa kwa kupigwa mkuki na
wafugaji ambapo hata hivyo Jeshi la Polisi lipo katika msako dhidi ya
wahalifu hao.
Wakati huo huo ,Jeshi hilo
linamshikilia Sijali Idd akiwa na Gobole moja ,unga wa baruti na gololi
11zinazotumika katika Gobole hilo.
Kamanda
Nyigesa,alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 4 mwaka huu saa 11
jioni katika Kijiji cha Msimbani Kata ya Miono Wilayani Bagamoyo.
Alibainisha
mtuhumiwa huyo alikuwa anatumia silaha hiyo kufanya shughuli za
uwindaji kinyume na utaratibu lakini atafikishwa Mahakamani mara baada
ya upelelezi kukamilika.
Katika hatua
nyingine,Nyigesa alitoa wito kwa wananchi kutii sheria bila shuruti na
kutoa taarifa za kiuhalifu kwa Jeshi hilo na vyombo vingine vya dola ili
wahalifu hao wachukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment