HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 10, 2021

ACT yapinga ongezeko bei ya petroli, dizeli Zanzibar


 

Na Mwandishi Wetu, Unguja

Chama cha ACT Wazalendo kimeeleza kushtushwa na mwenendo wa upandaji wa bei ya mafuta ya petroli na dizeli zinazotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZIRA) kila mwezi.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT Wazalendo, Salim Bimani leo Septemba 10, 2021, imeitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuangalia upya mfumo wa kodi za serikali katika sekta ya nishati ya mafuta kwa kutazama gharama za uingizaji wa mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.

Bimani ameishauri SMZ kwamba hatua hiyo ilenge kuwapunguzia wananchi mzigo mzito wa maisha hususan wale wenye kipato cha chini nacha kati kwakuwa ndiyo wahanga wakubwa pale bidhaa zinapopanda na hivyo kusababisha kuongezeka kwa mfumko wa bei kila mara.

"Kwa muda wa miezi 9 mfululizo, bei ya mafuta Zanzibar imekuwa ikipanda kila mwezi jambo ambalo si la kawaida kuwahi kutokea hapa nchini.

"Jambo hilo limepelekea ongezeko la wastani wa Sh 579 kwa lita moja ya petroli kutoka bei ya Januari ya Sh 1,882 hadi mwezi Septemba mwaka huu bei hiyo imefikia wastani wa Sh 2,461 ambalo ni ongezeko la Sh 506 kwa lita ya dizeli kutoka Sh 1,820 mwezi Januari hadi kufikia Sh 2,326 mwezi huu."amesema Bimani.

Aidha Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amesema kuongezeka kila mara kwa bidhaa hiyo ya nishati ya mafuta kumesababisha baadhi ya wafanyabiashara wa masoko ya Kibandamaiti na Jumbi kushindwa kuendelea na shughuli zao kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

No comments:

Post a Comment

Pages