Makamu wa Rais wa Mashindano hayo, Jolly Mutesi, Muaandaji, Rena Callist pamoja na Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Matiko Mniko wakiwa wamesimama mbele ya ya Gari aina ya Nissan X Trail atakalokabidhiwa Mshindi wa Kwanza.
Makamu wa Rais wa Mashindano ya Miss East Africa 2021 akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mashindano hayo yanayatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Novemba.
Muanzilishi na Muaandaji wa mashindano hayo kutoka Kampuni ya Rena Events Ltd, Rena Callist akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam.Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Nchi
16 za Ukanda wa Afrika ya Mashariki zimethibitisha kushiriki Mashindano
ya Miss East Africa 2021 yanayotarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu
jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Akizungumza na
wanahabari leo jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais wa Mashindano HAYO
kwa mwaka huu, Jolly Mutesi amesema mashindano ya Miss East Africa n
makubwa katika ukanda huo na kwamba yatatoa fursa ya kuitangaza nchi
kiutalii pamoja na kuonyesha fursa mbalimbali za uwekezaji.
Amebainisha
kuwa makampuni mbalimbali ndani ya ukanda huo yanatakiwa kutumia fursa
ya mashindano hayo kutangaza biashara zao ndani na nje ya mipaka ya nchi
kupitia shindano hilo.
"Mashindano haya
yatakuwa endelevu yatafanyika kila mwaka yatasaidia katika kudumisha
umoja wa nchi hizo, kukuza utalii, kutangaza fursa za uwekezaji hasa kwa
nchi iliyoandaa," amesema Jolly.
Amesisitiza
kuwa mashindano hayo yalibuniwa na Mtanzania Rena Callist na kufanyika
nchini kwa mara ya kwanza mwaka 1996 kwa mafanikio makubwa na kwamba
yamewahi kufanyika Burundi huku mara ya mwisho yalifanyika mwaka 2012
nchini Tanzania na kuangaliwa na mamilioni ya watu duniani kote.
Kwa
upande wake Rais wa Miss East Africa Beauty Pageant ambaye pia ni
Muaandaji wa mashindano hayo kutoka Kampuni ya Rena Events Ltd, Callist
amesema jumla ya ya zawadi zenye thamani ya Sh Mil 146 zitatolewa mwaka
huu huku Mshindi wa kwanza atazawadiwa Gari jipya la kisas aina la
Nissan X Trail toleo la mwaka huu lenye tamani ya Sh Mil 110.
Muuandaji
huyo amefafanua kuwa mshindi wa pili wa mashindano hayo ataPATA Zawadi
ya Sh Mil 11, mshindi wa tatu Sh Mil 5 na kwamba kutakuwa na zwadi
nyingine kwa washiriki za thamani ya Sh Mil 20.
Aidha,
amezitaja nchi zilzothibiisha kushiriki ni Tanzania, Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Ethiopia, Eriteria, Djibout, Somalia,
Malawi, Visiwa vya Shelisheli, Comoro, Madagascar, Reunion na Mauritius.
Pia
amesema washiriki wanatakiwa kuwa vigezo vikiwemo vya umri kuanzia
miaka 18 hadi 26, angalau elimu ya sekondari, uwezo wa kujieleza yeye
na nchi yake, urefu wa futi 5.8, mshiriki awe na tabia nzuri huku
akiwafahamisha warembo wanaotaka kushiriki kujisajili kwenye mtandao wa
mashindano hayo kwani watakaofuzu vigezo watafanyiwa usaili.
Naye
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Matiko
Mniko amesema mashindano hayo ni fursa ya nchi kutangaza vivutio vya
utalii na yataagaliwa moja kwa moja na watu 300 duniani kupitia vituo
vya runinga na mitandao.
Amewaomba wasichana
wenye vipaji vya urembo kujitokeza kwa wingi kushiriki kwani BASATA
itasimamia yale yaliyoainishwa katika mikataba pamoja na kusimamia
masilahi ya washiriki wa mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment