Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi
(wa pili kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya NMB Kama
Upepo inayolenga kuchagiza matumizi ya kadi za NMB mastercard na QR kwa
ajili ya kununua tiketi za ndege za Skylink.
Kutoka kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Skylink, Solomon Mwale,
Mkurugenzi wa Skylink, Moustafa Khataw na Mkuu wa Idara ya Biashara za
Kadi NMB, Philbert Casmir.
Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi
(wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Skylink, Moustafa Khataw wakizindua
kampeni ya NMB Kama Upepo inayolenga kuchagiza matumizi ya kadi za NMB
mastercard na QR code kwa ajili ya kununua tiketi
za ndege za Skylink.Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Skylink, Solomon
Mwale na kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara za Kadi NMB, Philbert
Casmir.
Dar es Salaam, Tanzania
Benki
ya NMB imezindua kampeni ya 'NMB Kama Upepo,' iliyotokana na
Makubaliano ya Kibiashara na Kampuni ya Skylink Travel & Tours,
inayojihusisha na uwakala wa tiketi za ndege - kuwazawadia washindi sita
na wenza wao safari iliyolipiwa gharama
zote kwa siku tatu nchini Dubai.
'NMB Kama Upepo' ni kampeni itakayoendeshwa kwa miezi
mitano, ikilenga kukuza matumizi ya kadi za NMB mastercard na QR Code
miongoni mwa wateja wa benki hiyo kwa ajili ya kununua tiketi za ndege,
ambako watapata punguzo la asilimia 60 ya ada
ya huduma (service charges).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa 'NMB Kama Upepo',
uliofanyika jijini Dar es Salaam , Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na
Biashara, Filbert Mponzi, alisema kampeni hiyo itakuwa na zawadi za kila
wiki na kila mwezi kwa wateja wa NMB watakaofanya
malipo ya tiketi za ndege kutoka Skylink kwa kutumia kadi za mastercard
na QR Code.
"Kadri mteja atakavyotumia kadi katika manunuzi ya
mitandaoni au kufanya malipo kupitia kadi za NMB kwenye tovuti ya
Skylink, ama mashine zetu za malipo (POS) zilizoko katika ofisi za
washirika wetu hawa, ndivyo atavyojiongezea nafasi za kushinda
zawadi kutoka kwetu.
"Katika kipindi chote cha kampeni hii ya NMB Kama Upepo,
inayoanza Septemba 1, 2021 hadi Januari 2022, washindi sita na wenza
wao (jumla watu 12), tutawazawadia safari iliyolipiwa gharama zote,
ikiwamo malazi kwa siku tatu huko Dubai, tiketi
za ndege za kwenda huko na kurudi nchini, pamoja na pesa za matumizi,"
alisema Mponzi.
Aidha, Mponzi alifafanua kuwa, NMB Kama Upepo ni kampeni
chanya yenye lengo la kupunguza matumizi ya pesa taslimu na kwamba iko
wazi kwa wateja wote wanaomiliki kadi za NMB mastercard, sambamba na
wale wote ambao wameomba ama watakaoomba kadi
mpya wakati kampeni hiyo ikiendelea.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Skylink, Moustafa Khataw,
alisema Skylink ina furaha kubwa sio tu kuingia makubaliano ya
kibiashara na NMB, bali pia kuwa sehemu ya Kampeni ya NMB Kama Upepo, na
kwamba wateja wa benki hiyo watafurahia huduma chanya
zinazoenda kutolewa katika miezi yote ya uwepo wake.
No comments:
Post a Comment