-Kujenga hoteli zenye hadhi ya nyota tano 'brand ya Kempinski kwenye Hifadhi za Taifa
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Wawekezaji
mahiri kutoka Taifa la Bulgaria ambao wanakusudia kujenga hoteli tatu
zenye hadhi ya nyota Tano za 'brand' ya Kempinski katika Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti, Manyara Tarangire na Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya
Ngorongoro, ikiwa ni matokeo ya Kampeni ya Royal Tour iliyoasisiwa na
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wake maalum na
Wawekezaji hao uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waongoza Watalii nchini Bulgaria ambaye pia ni Mkuu wa Msafara wa Wawekezaji, Lachezar Todorov akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro moja ya zawadi mara baada yq kufanya mazungumzo na Wawekezaji mahiri kutoka Taifa la Bugaria ambao wanakusudia kujenga hoteli nne zenye hadhi ya nyota Tano katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Manyara , Tarangire na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro katika mkutano wake maalum na Wawekezaji hao uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro (wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawekezaji mahiri kutoka Taifa la Bulgaria ambao wanakusudia kujenga hoteli nne zenye hadhi ya nyota Tano katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Manyara Tarangire na Malmlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya mkutano wake maalum na Wawekezaji hao uliofanyika Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waongoza Watalii nchini Bulgaria, Lachezar Todorov na kulia wa nne ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo , Dkt.Allan Kijazi
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Allan Kijazi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Utalii Africa, Cuthbert Ncube ambaye ni miongoni mwa Wawekezaji kutoka Taifa la Bugaria, ambaye wanaokusudia kujenga hoteli nne zenye hadhi ya nyota Tano katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Manyara, Tarangire na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro katika mkutano wake maalum na Wawekezaji hao uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Maalum
SHUGHULI
za Royal Tour zilizokuwa zikifanywa kwa mara ya kwanza nchini na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan za
kutangaza vivutio vya Utalii, Biashara na Uwekezaji nchini zimeanza
kuzaa matunda kwa wawekezaji kuanza kujitokeza kwa uwekezaji wa hoteli
za kisasa ndani ya hifadhi za Taifa.
Hayo
yamebainishwa na Serikali kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro mara baada ya mkutano wake maalum na
Wawekezaji uliofanyika Dar es Salaam mapema leo
Ambapo
amekutana na wawekezaji hao kutoka Bara la Ulaya katika nchi ya
Bulgaria watakaojenga hotel za Nyota tano 'brand' za Kempinski kwenye
hifadhi Nne za Taifa nchini.
Waziri
Dk. Damas Ndumbaro amesema mpango mkakati wa Mhe Rais Samia Suluhu
Hassan kupitia kuandaa kipindi cha Royal Tour umeweza kuzaa matunda hayo
na wao kwa Wizara wameupokea kwa kwa sasa ni utekelezaji.
''Juhudi
kubwa za kimkakati za Royal Tour zilizoendeshwa na Rais wetu zimeweza
kuzaa matunda ambapo leo tumepokea wawekezaji mahiri kutoka Bara la
Ulaya ambao watawekeza kwenye hoteli kwa kujenga hoteli tatu za nyota
tano za 'brand' ya Kempinski kwa uwekezaji wa Dola za Kimarekani
Milioni 72. [USD 72 Milioni].
''Mkutano
wetu huu hii leo umekwenda vizuri sana na Wawekezaji hawa kwa hiyo
unaweza kuipata hoteli ya Kempinski baada ya ujenzi huo kukamilika. ..
Kempinski Serengeti, Kempinski Manyara, Kempinski Tarangile na
Kempinski Ngorongoro." Alisem Dk. Ndumbaro.
Waziri
Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa, ujenzi huo ni mkubwa sana na
unakadiriwa kuanza rasmi mwezi Januari 2022 ambapo amemshukuru kwa mara
nyingine Mhe Rais kwa kuwezesha kuwapigia 'pass' na wao kupitia wizara
ya Maliasili ni utekelezaji ikiwemo kupokea Wawekezaji katika sekta hiyo
ya Utalii.
''Tunaenda
kasi tayari hii Royal tour kwangu mimi kama Waziri na Wizara ya Utalii
na Maliasili kwa ujumla wake tunaichukulia kama 'pass' ya mwisho katika
mpira, unapopewa pasi ya mwisho kazi yako wewe ni kufunga tu. Kwa hiyo
sisi tumeshafunga 'Goal' lingine hilo kuhakikisha kwamba Royal Tour
inakuwa na mafanikio zaidi'' alimalizia Waziri Dkt. Damas Ndumbaro.
Agosti
28, mwaka huu Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alianza rasmi kurekodi
vipindi vya Royal Tour maeneo mbalimbali ya vuvutio vya utalii na
uwekezaji ikiwemo Tanzania Bara na visiwa vya Zanzibar.
Ambapo
katika ziara hiyo ya kuandaa vipindi hivyo kutembelea na kuonesha kwa
wageni vivutio mbalimbali vya Utalii, Uwekezaji, Sanaa na Utamaduni
vilivyopo nchini na kwa sasa matunda yake yameanza kuonekana.
No comments:
Post a Comment