HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 12, 2021

VIONGOZI WA TAASISI MBALIMBALI NCHINI WATAKIWA KUHESHIMU MISINGI YA UTAWALA BORA

 

Mwezeshaji na Mshauri Mwelekezi wa Utawala Bora Wakili Lawrence Chuma akisisitiza jambo kwa washiriki.

 

NA STEPHANO MANGO, SONGEA

VIONGOZI wa Taasisi mbalimbali wamekumbushwa kuheheshimu misingi ya utawala bora pindi wanapotoa huduma kwa waliowapa dhamana kwa kufuata taratibu,kanuni na sheria za nchi ili waweze kuleta matokeo chanya kwa jamii ambayo imekusudiwa.

 

Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji na Mshauri Mwelekezi Utawala Bora Wakili Lawrence Chuma katika warsha ya Utawala Bora iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma hivi karibuni na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa utawala bora.

 

Wakili Chuma amesema Viongozi wa Taasisi mbalimbali wametakiwa kuzingatia sheria,kaninu na taratibu za utawala bora na  uwajibikaji katika kuwatumikia wananchi kwa lengo la kuwajengea wananchi misingi imara ya kuwabijika na kushiriki kuijenga nchi yao katika Nyanja mbalimbali.

 

“Viongozi mmepata dhana ya kuongoza wananchi hivyo mnapaswa kuzingatia misingi ya utawala bora kwa kutoa taarifa sahihi na kwa kutumia lugha nyepesi ambayo itawezesha wananchi kuwa na uelewa wa kutosha”.amesema Wakili Chuma.

 

Wakili Chuma ameongeza kwa kusema utawala unaozingatia demokrasia,uwajibikaji,ushirikishwaji, maridhiano,haki za binadamu na utawala wa sheria unatoa fursa kwa wananchi kunufaika na rasilimali za nchi kwa pamoja.

 

Kwa upande mwingine Wakili Chuma amewataka wananchi kuwajibika kikamilifu katika swala zima la kulinda,kusimamia na kutunza rasilimali za nchi ili ziweze kutoa huduma endelevu kwa vizazi vijayo.

 

Kwa upandewake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la Millenium Art Group Mnung’a Shaibu Mnung’a ametoa wito kwa viongozi kuwajibika kwa wananchi kwa kuwapa taarifa sahihi kwakuitisha mikutano ya hadhara ambayo inatoa fursa kwa wananchi kujadiliana na kuamua kwa pamoja katika kutekeleza mipango yao.

 

 “Tunasisitiza sana viongozi kuitisha mikutano ambayo hailengi tu kuwapa taarifa wananchi kuhuhsu michango na maelekezo mbalimbali “amesema Mnung’a

 

Amesema wananchi wamekata tamaa ya kwenda kushiriki mikutano ya hadhara kwakujenga dhana ya kwamba kwenye mikutano hiyo agenda ni kupatiwa taarifa za michango mbalimbali na maagizo ya jambo fulani.

 

Kufuatia hali hiyo Mnun’ga ametoa wito kwa viongozi wa taasisi mbalimbali kuwajibika kutoa elimu kwa wanachi katika kuwashirikisha na kujadili kwa pamoja mipango inayopangwa na serikali na utekelezaji wake ili wananchi nao washiriki kikamilifu.

 

Millenium  Art Group Shirika lisilokuwa la kiserikali limeendesha mafunzo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambao nao wanatakiwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora.

MWISHO

No comments:

Post a Comment

Pages