HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 12, 2021

KITUO CHA MAFUNZO CHA KULINDA AMANI CHAFUNGA KOZI YA UKOMANDO DAR

 NA CAPT. SELEMANI SEMUNYU


MKUU wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu,  Brigedia Jenerali Iddi Nkambi, amefunga Mafunzo ya Makomando wa Jeshi la Wananchi Tanzania na wale wa Marekani yaliyofanyika kwenye Kito Cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Kunduchi jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza mara bàada ya kufunga Mafunzo hayo, Brig. Jenerali Nkambi alisema mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuunganisha nguvu kati ya Tanzania na Marekani katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kimataifa, ikiwemo ugaidi vinavyotishia ulimwengu kwa sasa.

 

Kwa upande wake, KamandaKikosi Cha Makomando wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Liteni Kanali Clif Kulya, alisema mafunzo hayo yamehusisha Maafisa na Askari wenye Taaluma Maalum ya Ukomando na yametoa fursa kujifunza kwa pande zote mbili namba ya kukabiliana na uhalifu usiojali mipaka ya nchi.

 

Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi Julai 28 mwaka huu na Mkuu wa Kamandi ya Afrika wa Jeshi la Marekani, Jenerali Stephen Townsend na kuhitimishwa Septemba 10.

No comments:

Post a Comment

Pages