Waziri wa Mawasilano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndungulile, akizungumza na Kaimu postamasta mkuu wa shirika hilo alipotembelea kaunta za vituo vya huduma ya pamoja.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza na wanahabari kuhusu kuelekea Uzinduzi wa Vituo vya Huduma ya Pamoja utakaofanyika Viwanja vya Posta Kuu Septemba 6 mwaka huu.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa
Vituo vya Huduma Pamoja (One Stop Service Centres) ndani ya Shirika la
Posta Tanzania (TPC) utakaofanyika Septemba 6 mwaka huu katika Viwanja
vya Posta Kuu jijini Dar es Salaam
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari Dkt. Faustine Ndungulile wakati akizungumza na wanahabari kuhusu
huduma zitakazopatikana kwenye vituo hivyo pamoja na maboresho
yaliyofanyika kwenye shirika hilo.
Amesema kuwa
vituo hivyo vikizinduliwa itakuwa ni utekeleza wa Ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) inayosisitiza utoaji huduma bora za posta kwa wananchi
ambazo zitapunguza foleni katika taasisi za umma wakisubiri kupatiwa
huduma.
" Tunaenda kuzindua huduma ya pamoja
tunafanya hivi kutekeleza ilani ya CCM hatutaki wananchi wapange foleni
tunataka wapate huduma bora bila hilo kutokea siku ya jumatatu Waziri
Mkuu atazindua vituo katika Jengo la Posta," amesema Dkt. Ndungulile.
Amebainisha
kuwa ndani ya vituo kutapatikana huduma za taasisi mbalimbali zikiwemo
uhamiaji, usajili wa vizazi na vifo (RITA), usajili wa makampuni na
majina ya biashara (BRELA), huduma za utambulisho wa namba za mlipa kodi
(TIN), Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Bima ya Afya (NHIF), halmashauri
pamoja na huduma za wastaafu.
Amesisitiza kuwa
vituo hivyo vitaanza katika mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma na kwamba
awamu ya kwanza itahusisha mikoa 10 ambayo ni Arusha, Kigoma, Mbeya,
Zanzibar, Morogoro, Lindi na Tanga.
Ameongeza
kuwa tayari zimetengwa Dola Mil 150 kwa ajili ya Mradi wa Tanzania ya
Kidijitali na kwamba kuna fedha zitaingizwa katika uboreshaji vituo
hivyo huku akikazia baadaye kutakuwa na dirisha moja litakalotoa huduma
hizo.
Amefafanua kuwa ndani ya miezi tisa
serikali imefanya maboresho mbambali ikiwemo kulilifua upya shirika
hilo, kuanzisha posta ya kidijitali pamoja na biashara ya mtandao ambapo
wajasiriamali 300 wamejisajili na kuunganishwa katika posta laki sita
na kwamba mtu akijisajili anapata faida ya bidhaa zake kuonekana dunia
nzima pamoja kutatua changamoto ya wizi wa mtandaoni.
Katika
hatua nyingine Dkt. Ndungulile amesema shirika la posta limeendelea
kutambulika duniani hivi karibuni baada ya kushinda nafasi mbili ikiwemo
ya Baraza la Utawala na Uendeshaji huduma za posta zote zikitolewa na
Shirika la Posta Duniani.
Dkt. Ndungulile
amesema kampuni zote za simu zimepewa utaratibu wa kuwasiliana na wateja
kwa kutumia namba 100 na si vinginevyo hivyo mteja atakayepigiwa
tofauti na namba hiyo atoe taarifa ili hatua zichukuliwe.
Kwa
upande wake Kaimu PostaMasta Mkuu wa shirika hilo, Macrice Mbodo
amesema awamu ya kwanza ya vituo hivyo mwezi Disemba mwakani, awamu ya
pili itahusisha kuunganisha mifumo ya taasisi katika dirisha moja
itaanza Januari mwaka 2023 hadi Januari, 2024.
Amesema
vituo 17 vitaongezwa katika awamu ya pili ikihusisha Mkoa wa Pwani,
Iringa, Tabora, Kagera, Rukwa, Simiyu, Mtwara, Manyara, Songwe, Katavi,
Njombe na Geita.
Pia amesema awamu ya tatu ya
vituo hivyo itaanza mwezi Julai 2024 hadi 2025 na huduma zitahamishwa
kutoka ngazi za wilaya hadi mikoa.
Aidha,
amesema kuwa kupitia huduma mpya zilizoanzishwa ikiwemo duka mtandao
shirika hilo linapata aslimia 3% na mwenye duka anapata asilimia 97% na
kwamba huduma za posta kiganjani ambazo hutumia simu janja zimeingiza
zaidi ya Sh bilioni 3.
No comments:
Post a Comment