Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya ameipongeza Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini (TMA) kwa kuwa miongoni mwa mamlaka inayofanya kazi bora zaidi kwa kutoa taarifa zinazosaidia sekta mbalimbali hapa nchini.
Mhandisi Kasekenya amesema hayo, Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 15.2021 wakati akifungua mkutano wa 14 uliokutanisha taasisi na mamlaka mbalimbali zinazohusu masuala ya Uchukuzi kwa lengo la kupima utendaji kazi wa sekta ya Uchukuzi.
Amesema Taasisi hiyo imesaidia kutoa utabiri wa hali ya hewa kwa nchi nyingi zinazoizunguka Tanzania ikiwemo kuepuka athari mbalimbali.
" Taasisi hii ina muhimu mkubwa sana kutokana na kutoa taarifa kwa sekta zote hapa nchini kwani usaidia kutambua majira gani ujenzi unapaswa kufanyika zaidi"amesema Mhandisi Kasekenya
Akitolea mfano amesema hata naodha wa meli anapoendesha chombo hicho umlazimu kwanza kujua na kupata taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Hali ya hewa nchini(TMA).
Amebainisha kuwa Taasisi hiyo imepata bahati ya kuongozwa na Mwanamke ambaye pia amekuwa mshauri mkuu wa Rais wa hali ya hewa duniani.
Mhandisi Kasekenya amefafanua kuwa miradi mingi inapotekelezwa wahusika utakiwa kupata taarifa kutoka katika Mamlaka hiyo ili kuweza kutekeleza kwa ubora zaidi.
Amesema suala hilo ufanyika kisheria na uwa ni lazima kwani umtaka Mkandarasi wa ujenzi kutambua ni wakati ngani anapaswa Kutekeleza kazi hizo.
"Kunapofanyika ujenzi ni muhimu wakandarasi kutambua taratibu zote zinazofanyika ikiwemo kujua ni mazingira miradi hiyo inapaswa kufanyika"amesema
Akizungumza kuhusu mkutano huo Mhandisi Kasekenya amesema kila mwaka kumekuwa kukifanyika mkutano huo lengo kuu likiwa ni kufanya tathimini ya kazi mbalimbali ambazo zinafanyika katika sekta nzima ya Uchukuzi
Katika mkutano huo Taasisi mbalimbali ikiwemo za serikali na sekta binafsi za usafirishaji wa ardhini na majini ziliweza kushiriki kwa kujadili utendaji kazi katika ufanyaji wa Shughuli zao.
Awali Mkurungezi Mkuu wa TMA, Dkt Agnes Kijazi amesema Taasisi hiyo imekuwa ikitambua Shughuli za Uchukuzi kutokana na kuendana zaidi na masuala ya Utabiri wa Hali ya hewa .
Amesema kupitia mkutano huo wamefanikiwa kuonesha huduma mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na TMA katika miradi ya maendeleo katika sekta nzima ya Uchukuzi.
" Kupitia Maonyesho haya tunaonesha umuhimu wa kutumia Utabiri wa hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kutambua ni namna gani Utabiri wa Hali ya hewa unatolewa na kutumika katika sekta binafsi"amesema
Dkt Kijazi amebainisha kuwa katika kipindi hiki yapo mabadiliko makubwa ya Hali ya hewa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi .
Amesema kipindi hiki muhimu Shughuli za maendeleo kungalia masuala ya Hali ya hewa katika Shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
"Kwetu hii fursa muhimu kuonesha na kueleza huduma zetu ni kwa namna gani zinafanya kazi kwani TMA imeanzishwa kwa Sheria namba 2 ya mwaka 2019 pia ni takwa la kisheria huduma za Hali ya hewa ili kuhakikisha uwekezaji unakuwa endelevu"alisisitiza Dkt Kijazi
Aidha amesema Sheria hiyo uongoza matumizi ya Hali ya hewa jambo ambalo TMA inalifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment