Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani (Kulia) na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Group, Mhandisi Hersi Said (kushoto) wakionyesha mfano wa hundi ya mkataba huo uliosainiwa leo jijini Dar es Salaam.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kampuni
ya GSM Group, imeingia mkataba kwa miaka miwili na Ligi Kuu Tanzania
Bara wenye thamani ya Sh 2.1 kuwa mdhamini mwenza wa ligi hiyo.
Mkataba
huo umesainiwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) Athumani Nyamlani pamoja na
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni hiyo Mhandisi,Hersi Said.
Akizungumza
katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Mkurugenzi wa Uwekezaji wa
Kampuni hiyo, Mhandisi Hersi amesema kuwa utazinufaisha moja kwa moja
timu zinazoshiriki Ligi kuu Bara.
"
Kampuni ya GSM Group imeona kuna haja ya kuendelea kuisapoti tasnia ya
mpira wa miguu hapa nchini kwa kuongeza nguvu udhamini wa ligi jambo
hili litachochea ukubwa wa ligi yetu," amesema Mhandisi Hersi.
Amepongeza juhudi zinazofanywa na Bodi ya Ligi kwa kufaninikisha ligi kupiga hatua hivyo wadau wa soka wanatakiwa kuiunga mkono.
Amebainisha
kuwa kampuni hiyo imeamua kuwa mdhamini mwenza kutokana na imani na
uongozi wa sasa wa TFF huku akiongeza kuwa ana imani mkataba huo
utakwenda vizuri.
Amesisitiza kuwa mkataba huo
hauna mahusiano yoyote na klabu zilizozo chini ya udhamini wa kampuni
hiyo na kufafanua hakutakuwa na upangaji wa matokeo bali umelenga uona
kuondoa changamoto za kiuchumi ya timu zinazoshiriki.
Kwa
upande wake, Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Nyamlani ameishukuru
kampuni ya GSM Group kua mdhamini mwenza ambao wameufanya kwani una
manufaa kwa timu zilizo ligi kuu kutatua changamoto mbalimbali na kwamba
uongozi wa TFF umejipanga kutumia vyema fedha za wadhamini.
Pia
amesema wadau wa soka wanatakiwa kuendelea kuiunga mkono kampuni hiyo
ili iendelee kuisaipoti ligi hiyo pamoja na kuwaomba wadau wengine
kujitokeza kuidhamini kwa kuiga mfano wa uwekezaji huo.
No comments:
Post a Comment