Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla.
Na Hussein Ndubikile, Daer es Salaam
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameziagiza Manispaa zote za mkoa
huo kuendelea kuwasisitiza Wafanyabiashara wadogo wadogo 'Wamachinga'
kwenda kwenye maeneo waliohamishiwa kufanya biashara zao.
Hayo
ameyasema leo jijini humo wakati akizindua Mk
akati wa Usafi na Uhifadhi wa Mazingira uliobeba kauli mbiu isemayo Safisha Pendezesha Dar es Salaam.
akati wa Usafi na Uhifadhi wa Mazingira uliobeba kauli mbiu isemayo Safisha Pendezesha Dar es Salaam.
RC Makalla amesema kuwa kampeni ya
kuwaondoa Wamachinga katika maeneo yasiyoruhusiwa imeafanikiwa asilimia
90 na kwamba kauli ameitoa kutokana na baadhi yao kuendelea kukaidi
kuondoka kwenye maeneo hayo hivyo ameziagiza manispaa kuwasimamia waende
walikopangiwa.
" Da es Salaam tumefanikiwa kwa
asilimia 90 kuwaondoa Wamachinga kwenye wasiotakiwa wale waliokuwa
hawalitakii mema jambo hili wameshindwa viongozi wao ndio waliosaidia
kufanikisha hili," amesema RC Makalla.
RC
Makalla ametangaza kuwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi iwe siku ya
kufanya usafi katika jiji hilo hivyo wananchi wanatakiwa kushiriki
pamoja na kuwaagiza Wenyeviti wa Mitaa kutimiza wajibu kwa kuhamasisha
usafi katika maeneo yao.
Amewaagiza Wakuu wa
Wilaya zote kuwa waratibu wa usafi wa pamoja katika wilaya zao kwa
kuweka ratiba ya wananchi kushiriki kufanya usafi ili jiji hilo liwe
hali ya usafi.
Maagizo mengine ni taassi za
umma kulinda maeneo yao kisheria ili wasivamiwe na Wamachinga, majengo
yote umma, na binafsi kupigwa rangi,manispaa zote kupitia sheria
ndogondogo za ufanyaji biashara kiholela na utupaji taka pamoja na kutoa
vibali kwa kampuni za usafi zenye vigezo.
Amewaomba
viongozi wa dini kuwahamasisha waamini wao kufanya usafi kwani usafi
haliufuati itikadi za kidini hivyo dini zote zinahimiza suala hilo.
RC
Makalla amebainisha kuwa Disemba 4 mwaka huu wananchi jiji hilo
watasherehekea miaka 60 ya uhuru muda wa asubuhi kwa kufanya usafi
katika maeneo yao na kwamba jioni kutakuwa na burudani katika Viwanja
vya Leaders, Kinondoni.
Kwa upande wake, Katibu
Tawala wa Mkoa huo, Hassan Rugwa amempongeza RC Makalla kwa kuja na
mkakati huo na kusisitiza tayari wameshaanda mikataba ya utekelezaji
wake.
Nae, Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad
Mussa Salum amewahimiza wakazi kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kushiriki kufanya usafi kwani dini zote zinasisitiza usafi.
Baba
Askofu Jacob Sosthenes ametilia mkazo suala la ufanyaji ni la waamnini
wa dini kutokana maandiko ya vitabu vya dini kuwataka wanadamu kuwa
wasafi na kuhifadhi mazingira.
Mabalozi wa
Mkakati huo akiwemo Msanii Ali Kiba, Rajab Kahali' Harmonize' na Steve
Nyerere wamempongeza RC Makalla na kumuhakikishia kufikisha elimu ya
usafi na uhifadhi mazingira kwenye jamii.
Msemaji
wa Wamachinga wa Kariakoo Masoud Issa amempongeza RC Makalla na
kumuhakikisha wako tayari kuhamasisha wenzao kushiriki kufanya usafi
katika maeneo yao.
Amemuomba RC Makalla kutenga
stendi za magari katika maeneo waliyopelekwa Wamachinga ili wateja
waweze kufika katika maeneo yao kirahisi.
No comments:
Post a Comment