HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 06, 2021

BENKI YA CRDB YATOA ELIMU YA FEDHA KWA WAZAZI, WALEZI

Ofisa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo (kulia), Levina Anthony akitoa zawadi kwa mmoja wa wazazi aliyefungua akaunti ya watoto ya benki ya CRDB "Junior Jumbo Account" wakati wa tamasha maalumu lenye lengo la kuwajengea watoto utamaduni wa kuweka akiba wakiwa wadogo kupitia akaunti ya watoto ya Junior Jumbo Account na kuwashukuru wazazi na walezi kwa kuwafungulia watoto akaunti katika benki hiyo. Tamasha hilo lilifanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Ofisa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo, akizungumza katika tamasha maalumu lenye lengo la kuwajengea watoto utamaduni wa kuweka akiba wakiwa wadogo kupitia akaunti ya watoto ya Benki ya CRDB "Junior Jumbo Account". Tamasha hilo lilifanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Watoto wakicheza.
Baadhi ya wazazi na walezi wakiwafungulia akaunti ya watoto ya Benki ya CRDB "Junior Jumbo Account" wakati wa tamasha
maalumu lenye lengo la kuwajengea watoto utamaduni wa kuweka akiba wakiwa wadogo.

No comments:

Post a Comment

Pages