Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu Ludovick Utouh
amezindua Kitabu cha Ukaguzi wa Umma kilichopewa jina Misingi ya Ukaguzi
wa Umma (Principle of Public Sector Auditing) na kuwashauri watendaji
wa Serikali kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na CAG ili kuboresha
usimamizi wa Rasilimali za Taifa.
Kauli
hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati akizindua kitabu hiicho ambapo
amesema kuzinduliwa Kwa Ripoti hiyo kutawasaidia wananchi kuweza
kuelewa namna ya Rasilimali zao zinavyotumika katika kuwaletea
maendeleo.
"Ripoti
hii inaweza kutumika kama chanzo cha taarifa katika ufuatiliaji wa
matumizi na Rasimali za umma kuanzia ngazi ya halmashauri "Alisema
Mkaguzi mstaafu utouh.
Amebainisha
kuwa kipoti hiyo inafafanua umuhimu wa ukaguzi na maoni ya ukaguzi
pamoja na Mambo nane ambayo Serikali inatakiwa kuyafanyiakazi.
Ameyataja
mambo hayo ni pamoja na mwendo wa Hati za ukaguzi, mwendo wa
utekelezaji wa mapendekezo ya CAG sambamba na maagizo ya kamati ya
kudumu ya bunge ya usimamizi wa Serikali za Mitaa.
Mwandishi
wa Kitabu hicho Utouh amesema ameandika kitabu hicho baada ya kubaini
kuwapo uelewa mdogo na kukosekana vitabu katika eneo la taaluma yake
panapogusa mahususi ukaguzi hesabu za fedha kwenye sekta ya umma.
Akizungumza
kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Emmanuel Tutuba amesema kitabu hicho ni silaha muhimu kwa Serikali
kupambana na wabadhirifu wa fedha za umma.
Amemwomba
Utouh na Taasisi ya Wajibu anayoiongoza kukitafsiri kitabu hicho kwa
lugha ya Kiswahili ili kusaidia kila Mtanzania kukisoma na kukielewa kwa
wepesi.
Kwa
upande wake, Naibu Mkuu wa Ofisi ya CAG, Salina Mkumba amesema kitabu
hicho kimezingatia vigezo vyote vya kimataifa katika ukaguzi.
Nae,Mwenyekiti
wa Bodi ya Taasisi hiyo, Yona Killagane amebainisha kitabu hicho ni
silaha muhimu kwa Maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Maofisa
wa Ofisi ya CAG.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taasisi ya Uongozi, Balozi Ombeni Sefue amewataka viongozi
mbalimbali kuwa waadilifu na waaminifu wanapokuwa wakisimamia miradi ya
umma.
No comments:
Post a Comment