Meneja Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa, akibonyeza kitufe cha kompyuta kutafuta washindi wa droo ya NMB MastaBata Kivyako Vyako iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Mary Mwasikili na kushoto ni Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Pendo Mfuru. (Na Mpiga Picha Wetu).
Afisa Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Mary Mwasikili, akizungumza na mmoja wa wateja walioshinda katika droo ya pili ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa na kushoto ni Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Pendo Mfuru. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA MWANDISHI WETU
KAMPENI
ya 'NMB MastaBata - Kivyako Vyako', inayoendeshwa na Benki ya NMB
imeezidi kushika kasi ambako wateja 100 wa Benki hiyo wametangazwa
washindi wa Sh. Milioni 10 za droo ya wiki ya pili.
NMB
MastaBata ni kampeni inayolenga Kuhamasisha Matumizi na Malipo kwa njia
ya MasterCard, Masterpass QR na PoS, ambako NMB imetenga zaidi ya Sh
Mil. 200 zinazoshindaniwa katika kipindi cha wiki 10, huku washindi
wakipewa pesa taslimu ili kuwapa uhuru wa kujipangia matumizi.
Akizungumza
kabla ya droo ya Wiki ya Pili iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja
wa Kitengo cha Kadi wa NMB, Sophia Mwamwitwa, alisema kampeni hiyo
inapewa msukumo wa mahitaji ya ulimwengu wa kisasa unaoamini katika
matumizi yasiyohusisha pesa taslimu, ambayo yanakabiliwa na changamoto
kadhaa, zikiwamo za upotevu na wizi.
Aliongeza
kuwa, kutokana na uhitaji huo, NMB wakabuni kampeni hiyo ambayo
imefanyika kwa misimu mitatu sasa na kuchagiza ukuzaji wa matumizi ya
kadi, kiasi cha benki yake kutunukiwa Tuzo ya Benki Kinara wa
Uhamasishaji Matumizi ya Kadi mwaka 2021, ambako walikuza matumizi hayo
kwa asilimia 104.
"Kampeni
hii ilianzishwa mwishoni mwa Desemba mwaka jana na itaendelea kwa wiki
10, ambako zaidi ya washindi 1,000 watazawadiwa pesa taslimu. Tutakuwa
na washindi 100 wa kila wiki, washindi 25 wa kila mwezi ambao
watajishindia Sh. 100,000 kila mmoja, na katika 'Grande Finale' tutatoa
washindi 30 wa Sh. Mil. 3 kila mmoja.
"Wito
kwa wateja wetu ni kuendelea kutumia kadi zao kufanya malipo na
matumizi kwa MasterCard, Masterpass QR na Vituo vya Malipo vya NMB
(PoS), ili kujiongezea nafasi za kushinda. Wasio na kadi waziombe
matawini na wasiokuwa wateja wetu, watembelee matawi yetu kote nchini
wafungue akaunti, ili sio tu kushinda zawadi hizi, bali pia kufurahia
huduma zetu," alisema Mwamwitwa.
NMB
MastaBata - Kivyako Vyako inafanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ambapo droo ya pili ilikuwa
ikisimamiwa na Pendo Mfuru, aliyewahakikishia wateja wa NMB kuwa vigezo
na masharti vinazingatiwa katika kupata washindi wa kampeni hizo.
"Jukumu
letu kubwa ni kusimamia michezo hii na niko hapa kwa jukumu hilo na
niwahakikishie wateja wote kuwa kila kitu kinaenda chini ya utaratibu,
sheria na kanuni za GBT," alisema Pendo Mfuru kabla ya kuanza
uchezeshwaji wa droo hiyo ya pili.
No comments:
Post a Comment