Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dorothy Gwajima (wa pili kulia) akisali pamoja na waumini wa Kanisa la African Inland Church of Tanzania (AICT) Kizota, jijini Dodoma Januari 30, 2022. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Jinsia, Grace Mwangwa.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
VIONGOZI wa dini zote wametakiwa kushirikiana na Serikali kukemea vitendo vya ukatili katika nyumba za ibada kwa lengo la kuinusuru jamii na kwamba wanaofanya vitendo hivyo ni baadhi ya wanajamii waliokosa utu.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu Dk. Dorothy Gwajima ,katika ibada iliyofanyika Kanisa la Afrikan Inland Church Tanzania (AICT) Kizota Jijini hapa, amesema wanaofanya vitendo vya ukatili wapo katika jamii hivyo ni vema viongozi wa dini kwa nafasi yao wakakemea.
Dk.Gwajima ameeleza ni wakati wa jamiina wadau wakiwamo viongozi wa dini zotekushirikiana kutokomeza ukatili huo na serikali inatekeleza mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto.
"Serikali peke yake haiwezi kufanikiwa endapo makundi mengine katika jamii yataachwa nyuma hasa nyie viongozi wa dini kwa nafasi yenu naombeni mtusaidie ili kutokomeza vitendo hivi vya ukatili," amesema Dk. Gwajima.
Ameongeza kuwa aiku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya ya kutisha kwa watu kutoana uhai kwa sababu ambazo hazijulikani.
Waziri huyo amefafanua kuwa Serikali ina imani wanaofanya vitendo hivyo wako kwenye jamii na wote wana dini zao na kwamba rai kama serikali wanaomba Viongozi wa Dini kulibebe suala hilo kwa pamoja.
Aidha, ameongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ambayo ina dhamana la kushughulikia maslahi mapana ya jamii ikiwemo kukemea vitendo vyote vya uvunjifu wa haki na ustawi wa binadamu.
Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa hilo Mch. John Sweya amesema mauaji hayo ni kinyume cha haki za binadamu na maelekezo ya vitabu vitakatifu ambapo anayeweza kutoa uhai wa binadamu ni Mungu pekee.
Amesema vitendo hivyo vinasababishwa na wanajamii kukiuka maelekezo ya Mwenyezi Mungu yanayosisitiza upendo miongoni mwao.
Ameahidi kupitia kanisa hilo kushirikiana na Serikali kupitisha elimu kwa Umma kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili yakiwemo mauaji.
"Waumini tumrudie Mungu na kumuomba ili kutengeneza Taifa lenye upendo" amesema Mchungaji Sweya.
Kwa siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la baadhi ya watu katika maeneo mbalimbali ya nchi kuuana na kusababisha taharuki.
Serikali iliandaa na kutekeleza Mpango wa Tiafa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto MTAKUWWA wa mwaka 2017/18 hadi 2021/22 unaolenga kutokomeza vitendo vya ukatili kwa angalau asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.
No comments:
Post a Comment