HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 31, 2022

JIJI LA DODOMA LANUNUA VIFAA VYA UPIMAJI WA VIWANJA KWA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
 

JUMLA ya Sh. Milioni 240 zimetumika na JIJI la Dodoma  ambazo fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya upimaji wa viwanja   vyenye uwezo wa kupima viwanja 300 kwa siku .
 

Akizungumza Wakati uzinduzi wa Vifaa hivyo vya upimaji Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema vifaa hivyo vitatumika  kupima  viwanja vya Mkoa huo , lengo kuu ikiwa ni  kumaliza tatizo la Migogoro ya ardhi iliyo katika jamii.

Mafuru amesema migogoro mingi ya ardhi ilijitokeza miaka 2 hadi 3 iliyopita imesababishwa na makampuni ya upimaji kwa kutengeneza tamaa kwa kugawa viwanja vidogo vidogo ili wapate faida suala hili lilikuwa ni tatizo kubwa .


"Makampuni haya pia yalikuwa wakiwaacha vishoka wamekuwa wakibaki saiti na kuanza kufanya mambo yasiyoeleweka,"amesema Mkurugenzi huyo.

Sambamba na hilo amewatahadharisha watendaji hao kutoazimisha wala kukodisha vifaa hivyo vya upimaji katika mikoa mingine kwani vifaa hivyo ni kwa ajili ya kufanya kazi katika jiji la Dodoma peke yake na sio mikoa mingine.

"Kumbukeni vifaa hivi tumenunua kwa pesa za wananchi wa Dodoma wanaolipa mapato lakini pia tambueni vifaa hivi vimenunuliwa kwa bei kubwa tumetenga bajeti kwa muda mrefu na tumenunua hivyo tusikodishe vifaa hivi sehemu yoyote kila Halmashauri ina mapato yake wanunue vifaa vyao wenyewe na sio kuja kukodi kwetu," amesema Mkurugenzi Mafuru

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri ameitaka Sekta ya Upimaji iwe ni sekta ya kutoa huduma zaidi nakuacha kufanya biashara na Halmashauri ihame kwenye mtazamo wa kufanya biashara na watoe huduma kwani kwakufanya hivyo Migogoro ya ardhi itakuwa historia katika jiji la Dodoma .


Hata hivyo amesema kumekuwa na changamoto kubwa kwa watendaji wenyewe licha ya vifaa hivyo kupatikana lakini wajitume kwani vifaa vya kisasa wameshapatiwa na mwisho wa siku uongozi wa jiji utahitaji taarifa ya maendeleo na matokeo ya vifaa hivyo.

"Nyinyi ni watendaji na mmekuwa mkilalamikiwa sana sasa Mnao uwezo kubadilisha taswira iliyopo kutoka kwenye kundi la watu wanao lalamikiwa likiwa watu wenye mfano tunataka watu waone matokeo na kusiwe na urasimu wa aina yoyote na waende wakawaonyeshe watu maeneo yao  na wafungue barabara,"Amesema  Shekimweri.

No comments:

Post a Comment

Pages