Askofu wa Kanisa la Pentekoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania Profesa.Rejoice Ndalima ambaye pia ni mwanasaikolojia akifafanua jambo kihusu mila potofu za kumuweka mtoto ndani kwa muda mrefu.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
UTAFITI unaonesha kuwa mtoto anaekaa ndani muda mrefu bila kutoka nje akitoka inakuwa ni tatizo kwa wenzake na akili zake zinakuwa hazijachangamka.
Kuna baadhi ya wazazi,walezi wanamila potofu za wanawafungia watoto wao wadogo ndani hadi atakapo anza shule darasa la awali wasicheze nje na wenzao jambao ambalo linamsababishia mtoto huyo kupungukiwa na baadhi ya vitamini D vinavyotokana na jua.
Hayo yamesemwa leo na Askofu wa Kanisa la Pentekoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania Profesa.Rejoice Ndalima ambaue pia ni mwanasaikolojia wakati akizungumza na Habari Mseto Blog amesema mtoto huyo hawezi kujiamini, mwoga, hawezi kujenga hoja wala kujilinda.
Prof. Ndalima ameeleza kuwa mtoto anayefungiwa ndani baadae atakuwa mbaya kwani mtazamo wake wake anafikiri watu wote ni kama wazazi wake aliyewazoea.
Amesema kuwa kumtoa mtoto nje kuna faida nyingi kiafya kwani jua la asubuhi na jioni lina vitamini D.
"Ufahamu wake unakuwa umefungiwa kama kwenye kibuyu mtoto atakiwa atoke nje kuzecha na wenzake," amesema Prof.Ndalima.
Ameongeza kuwa hali ya hewa ya nje ni nzuri kuliko ya ndani ambapo pengine kuna Kiyoyozi "Air Condition" kiafya haimsaidii bali mtu hujisikia vizuri kwa kuwa mtu anakaa sehemu amabayo anajisikia vizuri hakuna joto.
Prof. Ndalima amefafanua kuwa hali ya hewa ya nje inajenga kinga za mwili na kwamba kinga hiyo hujengwa na mazingira ya asili.
No comments:
Post a Comment